Tofauti ya Bongo Fleva/Hiphop ya zamani na sasa.’’Media’’

 

radio-microphone

Tofauti ya Bongo Fleva/Hiphop ya zamani na sasa.’’Media’’

Miaka ya 1994 ndio miaka ambayo Bongo Fleva/hiphop Ilianza kuchezwa katika kituo cha Radio One ambapo kwa mujibu wa historia Taji Liundi na Mike Mhagama ndio waliokuwa watangazaji wa kwanza kucheza nyimbo hizi kwenye kipindi cha Dj Show.

Kuna muda yatupasa tusiogopane kuambiana ukweli ili tuweze kujenga misingi ya yenye maana na furaha katika maisha yetu lakini pia mafanikio.Uongo umekuwa mtamu na mzuri zaidi kwa walio wengi waliopo kwenye media.

 Hii nimeamua kuandika bila kujali nani atanichukulia vipi, ila kwenye ukweli daima nitasema tu. Nikisema media hapa nagusa maeneo yote kuanzia ngazi ya Radio, Runinga, Blog, Gazeti na nyingine nyingi maana nyakati zimebadilika.

Watu hawa hawako kama ambavyo ilikuwa zamani, sipingi!! kweli nyakati zimebdilika na itashangaza kupinga mabadiliko. Lakini uhalisia wa zamani ilikuwa ili msanii usikike katika vituo vya habari ni lazima uwe na kazi nzuri na yenye ubora.

Ila sasa ni tofauti kabisa watangazaji na madj hawazingatii kazi nzuri bali urafiki, umkoa, na unafiki wa kiwango cha juu.
Jambo hili limeendelea kukua na limefika pazuri maana sasa tunawasikia wale wale ambao katika uhalisia si wenye vipaji hivyo ambavyo husifiwa.
Unafiki huu ni ngumu kuisha, mara pale msanii anaposema tu juu ya unafiki huu basi kifungo cha kutokupiga nyimbo ndicho hufuata.
Nash mc aliwahi kusema katika wimbo wake wa Tunazindua Mitaa aliyomshrikisha One Incredible, Stereo na P the Mc. Nash alisema “Refa anapendelea ukiongea unapewa kadi’’

Katika uhalisia watu wengi wa media sasa wanapenda kuabudiwa, na hata anapokuwa anamhoji msanii mtu wa media hujiona yeye ni maarufuku kuliko msanii.

Lakini pia hata msanii akiwa anawapa changamoto katika kujibu maswali basi husema “Anajifanya mjuaji yule”na hapo ni ngumu tena kusikia amepewa mahojiano.

 Licha ya hivyo pia kasumba ya kutaka kupostiwa katika sherehe zao za kuzaliwa imekuwa kubwa mno eti siku hizi usipomposti pia ni tatizo.
Mambo haya si ya kuficha ni ya kuweka wazi, maana haya yanafanya wasanii wenye vipaji vya kweli ambao hawako tayari kufuata matakwa ya watu wa media kama vile hongo, ushikaji, na mengine kutosikika kama wale wengine ambao wameamua kumtumikia kafiri ili kupata ujira wao.

Imefika wakati sasa kuacha tabia za kutaka kumenejii maisha ya msanii, ni vyema mkatazama zaidi ubora wa kazi yake.

Kama kweli watu wa Media wataamua kufanya yale mazuri ambayo yalifanya enzi za kuamka kwa Bongo Fleva/Hiphop hakika tutafika mbali Zaidi ya hapa.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa