Tofauti tatu zenye utofauti wa Giggy Money.

Tofauti tatu zenye utofauti wa Giggy Money.

‘Kiki ni Giggy’ ni endelezo zuri lakini hekima ya sanaa imtawale. (Hakika)

Jambo gumu ni kujitafuta na kujijua wewe ni nani, na katika kujitafuta huzaliwa mengi huenda yakawa mazuri au mabaya. (Inategemea).

Katika mengi ambayo Giggy alikuwa akifanya nje ya muziki hata baada ya kuanza muziki sisi tunaamini ni katika kujitafuta.

Na hakika amejipata sasa kwenye muziki na ‘Kiki ni Giggy’ ni mpatio halisi ambao ni endelezo zuri toka wimbo wake wa ‘Nampa Papa’ na ‘Mimina’

Mdundo wa S2 Kizzy katika wimbo wa ‘Kiki ni Giggy’ unashawishi kwa mapana yake kusikia ambacho kimefanyika ndani. Ila kiitiko ambacho amesimama Whozu na Sanja ni nogesho tamu katika wimbo huu.

La!hasha namna ya Giggy alivyoweza kutulia na midondoko katika mdundo huu hakika ameweka ukamilisho wa wimbo kuwa na uzuri wa ujazo katika burudani kwenye sikio lenye usikivu.

Hatuwezi kuacha kusifu namna ya tofauti tatu zenye utaofauti wa Giggy katika sanaa ya muziki. Katika nyimbo tatu yani Nampa Papa, Mimina na Kiki ni Giggy ni ngoma tofauti katika tengenezo la mashabiki.

Sanaa ya muziki ni pana katika uwasilishi na sio wasanii wote wanaweza kubadilika katika aina tofauti, Naam! Giggy ameweza.

Na hakuna kingine ambacho zaidi Giggy anapaswa kuzingatia zaidi ya hekima ya sanaa kama msanii. (Uhalisi)

Maana taswira iliyoko kwa wengi ni mbaya juu yake, lakini akisimamia sanaa hakika atakuwa vyema.

Lakini mswahili hunena yakuwa “Kinolewacho hukata” Tafakariiii.!!!!

#TuzungumzeMuziki