TID ALIMUHITAJI FID Q KUBADILISHA MUONEKANO WA KUFUNGWA

MAISHA YA JELA

Ni wimbo uliorekodiwa mwaka 2007.siku tatu baada ya kutoka kifungoni/gerezani. Asingefunguliwa PINGU zake kama isingekuwa msanaha wa Mh JAKAYA M KIKWETE raisi mstaafu..Msamaha wa rais hutolewa siku ya UHURU NA JAMUHURI 9/12 ..

MAISHA YA JELA

Ni wimbo wa kweli unahusu uhalisia wa maisha aliyopitia akiwa kifungoni/gerezani.TID aliyaeleza maumivu,machungu ya moyo na masahibu aliyopata akiwa jela/gerezani kutokana na adhabu ndogo ndogo alizopata huko..

Ndani ya huu wimbo kamshirikisha rafiki yake wa muda mrefu FID Q.. Mtu amabae anamuunganiko wa kifikra za watu walio nje(huru kifira) na walio kifungoni (kifikra) na wale walio gerezani kabisa..
Alimuhitaji FID Q kumsaidia kubadirisha ulemuonekano wakifungwa na jamii ilivyomchukulia baada ya kutoka gerezani.. Hivyo alihitaji msaada wake katika kipindi hicho kigumu..

Wazo la kurekodi huu wimbo ilitolewa na mmiliki wa TONGWE RECS bwana JUNIOR MAKAME alimaarufu J MURDER …

Lakini walipomaliza kuutayarisha wimbo J-MURDER,FID Q na TID walikubaliana kutoutoa mapema.. Unaweza ukashangaa kwanini wameumiza akili kutunga na kurekodi lakini hakuwa tayari kuutoa!?
Tena walishauriana kuwa huu sio Muziki tu,ni Zaidi ya Muziki kwa wanzentu ambao wanaingalia haya tunayoyaandika na kuimbaa yamebeba ujumbe gani ndani yake.

Hao ni wale ambao wanajali na kusaidia wenzao wanao wazunguka.mabadiriko ya kimtazamo juu ya wenzao ni halisi/kiukweli na yanayoegemea/lenga kutokupoteza/haribu Furaha ya marafiki zao. Pia wanaamini wenzao wenye matatizo wanahitaji muda kuweza kuishi na wenzao tena (mtaani)..

Tarehe 13/02/2017 TID alijitokeza mbele ya vyombo vya habari kuomba radhi familia, ndugu na marafiki kutokana na kujihusisha kwa siri na matumizi ya MIHADARATI/DAWA ZA KULEVYA

” kuna matumaini na amani Zaidi kutubu makosa/madhambi kuliko kujipa UTAKATIFU BANDIA”

Ilituingia akilini sasa ni wakati sahihi wa kuuachia wimbo,na kutusaidia sisi na taifa letu.
Kama dunia haitaiga makosa basi wakosaji watafuta wao ni wapi walipikosea pakawafanya wakatumbukia kwenye madawa/mihadarati”

Tunatunaini/amini machungu/maumivu aliyopitia TID akiwa gerezani basi ni funzo.. Atarudi katika mstari ulionyooka na tuendelee kumuombea katika njia hii aliyoichagua kuifuata..