Tathimini halisi ya uzinduzi album ya Kitaa Olojia na upana wa Fid Q, Je! Iko na usawa?

Tathimini halisi ya uzinduzi album ya Kitaa Olojia na upana wa Fid Q, Je! Iko na usawa?

Usiku wa jana ni katika usikivu na uzinduzi wa album ya msanii Fid Q ambayo yaitwa Kitaa Olojia. (Naam)

Na ikumbukwe album hii ni subirio zaidi ya miaka 9 kwa mujibu wa wajuzi. Hatimaye jana ikawa imetimia. (Utokaji)

Album hii imebeba nyimbo 23, ambapo kati ya hizo 9 zilishatoka. Ambapo pia kwa wajuzi imeleta mgongano wa mawazo yakuwa “si album kamili kulingana na uwingi wa nyimbo nyingi kutoka” (Awali)

Sisi hatuna zaidi ya shukurani kuu kwa utokaji wa album hii. Kuhusu wajuzi tunajua kwa mapana yakuwa sheria zao zina ugumu. (Ufahamu)

Uzinduzi wa jana uliambatana na upana wa bendi ambapo si bendi yenye umoja lakini kusanyo lenye ujuzi katika burudani kuu. (Wajuzi)

Ambapo Solo Gita ni upigaji wa Emmanuel Gripa, Bass Gita ni John, wakati huo Kinanda ni Baraka na Drums ni Tito. (Mapigo)

Na waimbaji imara katika nagesho kuu ni Chris   Music, Gift, Karma pamoja na Shedrack. (Umoja)

Ukamili wa bendi umeleta Fid Q kufanya shoo yenye kiwango kikubwa kuliko. Na wajuzi hawakusita kusifu katika uwezo wa kutumia bendi. (Pongezi)

Lakini wajuzi wameweka wazi yakuwa “Fid Q ndiye msanii bora katika utumizi wa bendi” Sisi ni nani tupinge? (Ajabu)

Lakini fedheha ni namna ya Fid Q kushindwa kwenda na muda. Kwa kuchelewa kuanza shoo yake. (Soni)

Ilihali uzinduzi wa jana umefanya turejee andiko la zamani yakuwa “Fid Q anapaswa kuwa na upana wa shoo zake” (Uhalisia)

Kwa ukubwa wake wa sasa haipaswi kuwa ni msanii mwenye subirio la barua pepe au simu toka kwa promota. (Soni)

Bali uwepo wa shoo zake chache na kubwa zenye burudani kuu na ujazo kamili wa bendi toka kwake.(Hakika)

Maana vigezo vyote ya ukubwa anavyo, vivyo ni muda na maamuzi sahihi. Lakini pekee yake hawezi bali timu ya wajuzi wenye ujuzi wa soko na muda. (Ufahamu)

Yote ya yote tunatoa pongezi kuu kwa Fid Q kwa kutoa album hii. Ni wazi tumefurahishwa na mno katika usiku wa jana, shoo yake imekua yenye ujazo na itaishi ndani yetu. (Hakika)

#MuzikiNiSisi  #KitaaOlojiaAlbum