Tanzania kuna mashabiki wachache mno wa muziki. (Kweli

Tanzania kuna mashabiki wachache mno wa muziki. (Kweli)

Wasanii wengi hufarahia mno kuona namna wanapata wafuatiliaji wengi kwenye mitandao ya kijamii. (Iko Hivyo)

Na wengine hutamba mno kiasi cha kuanza kupagawa na namba za mtandao huku kileo cha dharau kikikoleo vyema. (Hakika)

Lakini katika uhalisi Tanzania mashabiki wa muziki au msanii husika ni katika uchache mno. (Kabisa)

Ipo mifano mingi mno katika thibitisho hili katika nyakati za sasa. Na ikumbukwe kipimo halisi cha mashabiki ni ununuaji wa kazi ya msanii hasa album. (Naam)

Miaka ya 2017-2019 tumeona wasanii wakijitahidi mno kwa kutoa album. Ambapo album kama Women ya Lady Jayedee, Above Inna Minute ya NavyKenzo, Money Monday ya Vanessa Mdee, Kisimani ya Wakazi, A Boy From Tandale ya Diamond Platnumz, Sam Magoli ya Nikki Mbishi na nyingine nyingi. (Album)

Lakini mapokeo ya uuzaji yakoje? hakika ni fedheha katika kweli yenye kweli. Na hii ni kulingana na namba za wafuatilijia za wasanii katika mitandao ya kijamii. (Soni)

Mashabiki wengi ni katika furaha ya matendo ya wasanii hasa yenye soni, si katika ununuzi wa kazi. Wengi mashabiki ni katika “Ebana noma sana, umependeza, na kujirekodi kipande cha wimbo ili msanii amposti. (Chekesho)

Mfano sasa tunaona msanii Maalim Nash Mc akiposti kwa upana juu ya album yake ya Diwani ya Maalim ambapo juhudi za kutangaza yapasa tumsifu vyema. (Pongezi)

Lakini muitikio ukoje ukilinganisha na wafuatiliaji ambao wapo nae katika mtandao wa picha tu Instagram? (Ulizo)

Si zuri kabisa ni lenye soni kwa mashabiki, mfano Maalim ana wafuatiliaji 82,000 kwenye mtandao wa picha instagram. (Ndiyo)

Kama wafuatiliaji hawa 82,000 kila mmoja akinunua album ya Nash kwa 7000 basi Maalim Nash atapata jumla ya 574,000,000. ‘Milioni Mia Tano Sabini na Nne'(Mafanikio)

Sasa huyo ni Maalim Nash katika wafuatiliaji wake, vipi kuhusu Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, na wengine wengi? (Ukubwa)

Vivyo basi ndiyo maana tunaona wasanii wa nje wakiishi kwa upana katika maisha ya sanaa kwa kuwa mashabiki wao ni wanunuzi kamili wa kazi za wasanii wao mara tu zitokapo. (Uhalisia)

Sisi Tanzania mashabiki wetu ni katika sifia tu za oya oya na upana wa matusi mengi yasiyo na faida wala maana lakini upana wa kusifu zaidi matendo si ununuzi wa kazi. (Ujinga)

Na mashabiki wetu ni hodari katika kicheko cha umasikini wa wasanii ilihali hawanunui kazi kabisa. (Upuuzi)

Ifike mahala mashabiki mlio wengi muunge wasanii mikono kwa kununua kazi zao kwa upana. Wasanii wetu wanafanya kazi kubwa vivyo wapeni muda mwema katika tulizo la ununuaji wa kazi. (Kabisa)

#MuzikiNiSisi