“Taa ya mtu mwenye mambo ya hovyo huzimika haraka” Amber Lulu

“Taa ya mtu mwenye mambo ya hovyo huzimika haraka” Amber Lulu.

Tulishasema yakuwa Amber Lulu ni mwanadada mwenye uwezo mkubwa wa kuimba, ila mapito yake ndiyo yenye kumpa tabu kwa mashabiki wa muziki kubadili mazoea ya tabia yake kuleta kwenye uhalisi wa muziki.

Lakini “kila jambo lina chanzo, ilihali mwisho unaweza usijulikane kwenye jambo lenye chanzo” (Uhalisia)

Hivyo Amber Lulu kwa sasa ilibidi abadilike katika mengi hasa kwenye kuchunga kinywa chake katika mahojiano mengi apatayo sasa.

Ni vyema kuzungumza kazi zake zaidi hasa muziki wake, na sio kuzungumza makalio yake au wasanii wengi kwa mlengo wa kuwadhalilisha ili yeye apate kuzungumziwa mtandaoni. (Ujinga)

Ni wazi haiwezi kumjenga kwa kukua kwa muziki bali kuzidi kufanya mashabiki wamdharau vyema.(Fedheha)

Taa yake ya muziki imewaka vyema sasa na mashabiki wamempokea vyema, hivyo kuendelea kuongea mambo ya hovyo itafanya taa yake izimike haraka. (Dharau)

Ni vyema autumie wakati huu vyema katika kujenga msingi imara katika safari yake ya muziki. (Kweli)

Ila nyakati zote mswahili hunena yakuwa “Mtembea peku hapendi, ila hana viatu” (Akili)

Na mswahili hakuacha kunena yakuwa “Mpiga ukuta ngumu, huumiza mkonowe” (Tafakari)

Nasi hatuwezi acha kusema kweli ilihali ya wengi kutoelewa kweli yenye kweli yenye uhalisi wa kubadili mengi yenye maana.

Nyakati hupita kiwepesi mno, hivyo kutumia wakati katika kufanya yenye maana ni jambo jema zaidi.

Amka Amber Lulu wakati ndiyo huu, na bila umakini utapita kiwepesi kama pepo za bahari ya hindi.

#TuzungumzeMuziki