Sumaku ya Jux na Vanessa Mdee ni ya wakati wote. (Eeh)

Sumaku ya Jux na Vanessa Mdee ni ya wakati wote. (Eeh)

Pendezo kuu letu ni badiliko la Jux katika uimbaji mzuri si katika mtiririko ule akiwa na mtayarishaji Maneck. (Mfanano)

Ni wazi kufanya kazi hii ya Sumaku na mtayarishaji S2kizzy kumeleta tofauti ya Jux nzuri yenye ujazo mpana wa uimbaji.(Hakika)

Lakini nogesho kuu ni vile Vanessa Mdee alivyopita juu ya mdundo katika verse ya pili. Hakika amepoa vyema katika usikivu imara. (Uimbaji)

 

Ingawaje ni kama kwenye wimbo huu kuna sauti za nyuma za G Nako katika usikivu, ni wazi zimeleta utamu mkuu wa wimbo huu. (Dhanio)

Lakini hatujasahau sauti za nyuma ya wimbo huu za Vanessa Mdee ni wazi zimekoleza vyema uzuri wa wimbo huu. (Usikivu)

Ikumbukwe sifa kuu ya muziki ni uburudisho mkuu, vivyo wimbo huu ni katika wakati wote wa burudisho kwa maana ya asubuhi, mchana, jioni na usiku katika maeneo mengi zaidi. (Starehe)

Ikumbukwe zipo aina ya nyimbo ambazo zenyewe ni kwa wakati fulani si katika wakati wote. (Uhalisia)

Ila ni wazi Sumaku imekaa vyema, pongezi kwa S2kizzy kwa kuandaa mdundo mzuri lakini uimbaji mzuri wa Vanessa Mdee na Jux. (Hongereni)

Uzuri wa wimbo huu wala haukuhitaji kiki ya kuachana bali kutoka na kupata matangazo imara yenye uimara mkuu. (Ufahamu) 

Yote ya yote mnapaswa kujua yakuwa “Asali na shurubati, hayana ladha moja” (Muziki na Kiki) 

#MuzikiNiSisi