Sugu ameonyesha awali ni awali tu hakuna awali mbovu.

Sugu ameonyesha awali ni awali tu hakuna awali mbovu.

Kwa namna ya utulivu katika wimbo wake huu wa #219 na kuongea yake yenye uhalisia kumefanya sikio litamani kusikia mara kwa mara wimbo tangu kutoka kwake.

Na nyakati zote tungo zenye uhalisi wa maisha huwa ni bora, lakini ubora haukamiliki kama hakuna midondoko au mitambo ambayo ni ya kupoa katika elezo jema juu ya mdundo.

Na mdundo umekaa vyema toka kwa mikono ya Mr T Touch, na kwa mashabiki na wafuasi wa Sugu wanajua kabisa midundo ya namna hii ndiyo midundo halisi ya Sugu.

Wimbo ni mzuri na upo katika hali kamili ya Sugu, lakini Je!wimbo huu utapata nafasi kwenye Media? kwa maana ya Radio na Runinga?

Kwa uhalisi na upana wa Sugu kwenye wimbo huu ameonyesha yakuwa “Awali ni awali hakuna awali mbovu”

Tunaona yafaa kabisa Sugu kufanya walau album katika nyakati hizi, maana kuna nyimbo kama Hakuna Matata, Freedom na #219 sasa kwanini album isiwepo?
#TuzungumzeMuziki

Attachment