Stereo kaangukia katika mikono salama ya wcb

STEREO KAANGUKIA KWENYE MIKONO SALAMA YA WCB

NA JOHN SIMWANZA

Msanii wa hiphop Stereo ambaye ni miongoni mwa marapa bora ambao wamepata kuwepo katika ramani ya muziki wa kizazi kipya chini ya mwamvuli wa hiphop, ambaye sasa taarifa za yeye kusaini katika label ya Wasafi ni taarifa ambazo zimekuwa zikienea Zaidi.

Licha ya muhusika kukataa kuweka wazi na akidai kuwa mwenye mamlaka ya kuweka wazi taarifa hiyo ni Diamond Platnumz mwenyewe. Ila zipo dalili zote za Stereo kusainiwa Wasafi.

Lakini kusainiwa kwa Stereo kuna baadhi ya Mashabiki itawashangaza kwani hawakutegemea kama WCB wanaweza kumchukua msanii anae fanya mziki wa Rap kama alivyozoeleka Stereo

Rapper Stereo alianza kusikika na kutambulika katika Mziki wa Hip Hop akiwa Chini ya M -Lab Lebo ambayo ilikua ikisimamiwa na mtayarishaji Duke  Huku ikiwa na Wasanii kadha wa kadha  Wakiwemo Nikki Mbishi na One the Increadible, Grace matata Bila kusahau mkali wa RnB Ben pol. Uwezo waliokuwa nao wasanii wa Lebo ya M lab uliwafanya waweze kutambulika vizuri Zaidi katika  muziki wa kizazi kipya   na katika lebo hii  Stereo Alifanikiwa kutoa Album Ilikuwa iliyokwenda kwa jina la Africa Son mwaka 2012.

Kama ilivyo kwa kila lenye mwanzo huwa halikosi kuwa na mwisho Stereo  alimalizana na Duke na kuwa  msanii ambaye Hayupo kwenye Lebo yoyote  na kusimama yeye kama  yeye ambapo haikuwa rahisi sana kufanya vitu vyote  kwakuwa muziki unahitaji vitu vingi sana ikiwemo gharama  za kurekodi, kusambaza kazi  na kufanya video ambazo zitazidi kukukusanyia mashabiki na kupata shoo mbalimbali.

Kwakua kizuri ni kizuri na chenye ubora ni bora basi uzuri wa ku Rap na ubora wa kuandika Mashairi Ulimfanya Legendary Ambwene Yessaya AY Kumchukua Stereo na Kumsimamia katika Lebo Yake iliyokua inaitwa Unity Enterteinment nakufanikiwa Kufanya ngoma mbili ambazo ni Never let you down aliyomsirikisha Victoria Kimani na ilifanyika katika studio za Bongo Records chini ya prodyuza P Funk na  Usione hatari ilifanywa na Chizan Brain katika studio za Noize maker  aliomshirikisha Mwana lebo mwenzake Ben Pol.

Track hizi mbili  zilisumbua sana chati mbali mbali za radio na Tv japo baadhi ya Wasanii wenzake hawakulibaliki swala la stereo kubadilika katika nyimbo hizi mbili lakini kwakuwa muziki unawigo mpana na ubora wa msanii ni kubadirika haikumyumbisha Stereo.

Stereo alimalizana na AY kwa ngoma hizo mbili  chini ya Unity Entertainment na kurudi tena kusimama kama jeshi la mtu mmoja huku akiwa karibu Zaidi na kufanya kazi na Familia kubwa Ya Muziki wa Hip hop ijulikanayo kwa jina la Tamaduni Muzik iliyo sheheni Wasanii wengi na wakali wanaofanya hip hop bila kuwasahau  Maswahiba wake wa muda mrefu Nikki Mbishi na One the Incredible na walikua na maonesho ambayo yalijizolea umaarufu mkubwa sana yaliyo kuwa yanafanyika kila Jumamosi katika ukumbi wa Msasani club.

Kutokana na Wadau wengi kuona muziki nakutambua madini yaliyopo ndani yake Stereo ndipo Raisi wa WCB Diamond Alipoamua kuvivaa viatu vya Duke na AY kwa wakati mmoja na kumchukua Stereo Mpaka katika Familia Iliyo sheheni Waimbaji Ambao hawata mpa Mawazo yakufanya Chorus na Melody kali ambazo pengine ingemuwia vigumu sana kuwapata kwa urahisi kama  ilivyo thamani yao Kwa sasa na kuna sababu za kusema kuwa Stereo Ameangukia Katika Mikono salama ya WCB.

Kwa Wasafi ni mahala ambapo wapo kibiashara Zaidi na kuwa na mikakati mizuri katika kumuweka msanii kibiashara Zaidi.

Leo hii tunaamini kabisa Stereo ameangukia katika mikono salama ambayo itampa mafaniko Zaidi ya awali. Hili lisifanye wale mashabiki wa hiphop wa Stereo kumchukia na kuona kama hayupo mahala salama, Team Tizneez tumezungumza na Stereo na kusema “Mimi ni yule yule na nitakuwa vile vile hivyo watu wasitegemee kuwa mtu wa tofauti Zaidi.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa