Stamina Ni vyema ukaacha unafiki mbele ya mashabiki.

Capture

Stamina Ni vyema ukaacha unafiki mbele ya mashabiki.

Ukweli hauna rafiki wala hauhitaji mtu, ukweli haupo upande wowote kati ya mke na mume, mweupe wala mweusi, daima ukweli hujitenga peke yake. Pia kuna wakati unaweza kuupenda ukweli na pia kuna wakati unaweza ukauchukia ukweli.

Kwanza kabisa nirejee kile ambacho amekipost msanii wa hiphop Stamina kupitia mtandao wa kijamii yani mtandao wa picha ‘Instagram”.

Katika posti yake ameandika “UJUMBE KWA ARTIST WENZANGU
tabia ya kutopeana tafu wenyewe kwa wenyewe ndo inaleta matabaka kwenye muziki

Mwenzako ana show sehemu, au ana nyimbo yake mpya anakutumia cover ya wimbo au ya show yake unaipata kabisa ila hutaki kupost tu.
Cha ajabu za wengine ambao ndo unaamini washikaji zako unazipost fresh tu kwa mbwembwe zote.
Mtu mpaka ana namba yako maana yake tayari mnajuana na mna ukaribu pia, hata kama hamna ukaribu ila sababu ni msanii mwenzie wee mpe tu support.
Mnasubiri mpaka mtu afariki/afe ndo mnajifanya kupost r. I. P wakati hawezi hata kuona hiyo post yako.
Mnasubiri mpaka mtu awe ameathirika na madawa, au kapigika kimaisha ndo mnajifanya kupost picha au viclip vya video na kujifanya mnahuzunika.
Me nikifa kausha tu usipost maana sitoona wala haitosaidia kama kipindi niko hai hukufanya hvyo.
#UNAFKI TU#”

Kwanza nianze na kueleza maaana ya neno “Unafiki” Maana ya neno hili ni hali ya kukuficha kwa makusudi kile kilichomo mawazoni/moyoni kwa lengo la kumwonyesha mtazamaji kuwa anachokiona ndicho, wakati ukweli wa mambo ni kwamba anachokiona ni tofauti sana na uhalisia.

Unafiki ni kama kuvaa gamba lisilo lako. Kubadili rangi ya mwonekano wako. Kuwa “artificial”. Unafiki ni kinyume cha uhalisi. Kwamba naweza kuigiza mwonekano fulani ambao kimsingi si wangu katika hali halisi. Naweza kumchekea mtu, wakati ukweli wa mambo ni kwamba ndani yangu nasikia kinyaa.

Katika hili ni wazi ikanifanya nirejee kwa Stamina yapo mengi ambayo amewahi kufanya nyuma ya pazia ambayo aliwahi kufanyia wasanii wengine na hata sisi Team tizneez.

Ila wakati akifanya hayo kwa upande wetu tulikuwa kimya na kuendelea na kazi yetu ya uandishi, lakini pia kuweka nyimbo zake pamoja na habari zake kuhusu muziki wake. Ila katika posti yake inashangaza kuona wasanii wenzake ni wanafiki alihali yeye ni kiongozi wa unafiki huo.

Ni muda kidogo sasa umepita tangu kutambulisha wimbo wa “Umeniroga”ambapo katika moja ya mahojiano yake Team tizneez ni watu ambao tulishoot clip za kutosha kwaajili ya kuweka katika mtandao wa “Youtube”. Na mara baada ya kukamilika zoezi hilo tulimtumia ili aweze kushare clip hizo ambazo kimsingi kwake zina faida kubwa mana ni katika kuendelea kutangaza kazi yake.Na kwa kuliona hilo hakusita hata kuomba kuwa mara tu ya zoezi kukamilika basi tuweze kushare nae video hizo.

Haikuwa ngumu kushera nae video clip hizo zilipokuwa tayari. Hakika ilikuwa kinyume na hakuna ambacho alikifanya kwa maana ya kupost kama alivyohitaji. Ila kwa kuwa www.tizneez.com ni blog inayoandika kuhusu bongo fleva na hiphop tuliweka mahojiano hayo ili kuendeleza dhamira yetu ya kusupport muziki huu wa kizazi kipya. Na hata tag katika mitandao ya kijamii katika kurasa zake tulifanya kwa kiwango cha juu, lakini hakuonyesha ushirikiano wowote ule. Je huo sio unafiki?

Ninaposema Stamina ni vyema aache unafiki mbele ya mashabiki nina maana kuwa, ilipaswa hata wale wasanii ambao wamekuwa wakimuomba awapostie cover zao alipaswa aposti sio kuanza kulalama mbele ya mashabiki ili aonekane mwema ilihali si mwema.

Lawama juu ya yeye kuposti kazi za wenzake zipo, achilia mbali wasanii wakubwa ambao Tanzania inawajua wapo wasanii wadogo ambao wapo mkoani Morogoro na hakika wamekuwa wakimtumia kazi zao Stamina ili aweze kutoa support ya kuposti tu lakini hakuwahi kufanya hivyo.

Kuposti katika mtandao wa kijamii ni kuwahi ili ajionyeshe mbele ya mashabiki kuwa yeye ni mwema na wasanii wengine ni wanafiki. Ingawa swala la unafiki lipo kwa wasanii wengi ila kwa leo tumeanza na Stamina maana ni moja ya watu ambao ameshindwa kuficha unafiki wake na kuposti kwenye mtandao.

Je ni kipi kinafanya alalamike leo hii? Ni vyema uishi maisha yako ni jambo baya na chukizo kuongopea mashabiki kama wewe ni mwema na kuona wengine ni wanafiki.

Nafikiri ni muda mzuri wa kuicha kama sio kupunguza tabia ya unafiki ambayo kama wewe utaweza kuikana basi naamini wasanii wengine wataweza pia kuikana kama sio kuacha.

Katika wimbo wake wa Mwambie Mwenzio katika verse ya pili alisema “Mabadiliko daima huanza na wewe” Hivyo vyema kuanza kuacha unafiki mbele ya mashabiki.

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez