Soni iwe juu ya wasanii wenye ubaguzi hodari kwa watu wa media. (Ujinga)

Soni iwe juu ya wasanii wenye ubaguzi hodari kwa watu wa media. (Ujinga)

“Asiyejua maana haambiwi maana” waswahili hunena hivyo lakini kwa hili hapana yapasa tunene na wajue maana katika uisho wa Sanaa kwa maana ya ndani na nje. (Muziki)

Sanaa imekua na ujazo wa wasanii ni wengi lakini lawama za ubaniwaji pia ni nyingi tena ni kila leo wasanii wengi hunena wanabaniwa, na imani ya ubaniwaji imekuwa kubwa mno. (Mashabiki)

Lakini ukimuuliza msanii unabaniwa wapi na nani? Hakika tajo lake ni kwa mtu mmoja au kituo kimoja tu. Ila uhalisi kuna vituo vingi vya habari na watu wa habari ni wengi sasa kwanini mmoja na kituo kimoja?. (Shangazo)

Ni kawaida kabisa kwa msanii kubagua mtu au kituo na kuthamini kingine tena kwa kelele fujo na mbwembwe. Na akitoswa huko huanza kupayuka mithili ya kuku aliyekosa pakutagia. (Upuuzi).

Ukichungunza wasanii wenye malalamiko zaidi ni wale wenye watu wao kadhaa mawazoni yakuwa hawezi bila ya Fulani au hawezi mpaka kituo Fulani. (Chekesho)

Anasahau yakuwa anapaswa kuwepo kila mahala katika vituo, hivi hawaoni mfano wa makampuni makubwa yapo kila kituo kwa maana yanaamini katika kila mmoja na upana wake. (Kabisa)

Wewe msanii ni nani kiasi uwe na baguzi hodari kwa mtu au watu wa vituo vingine?. Yapasa uwe kila kituo katika tangazo la kazi/biashara yako bila kujali mtu wala watu kadhaa. (Uthamani)

Vile ambayo msanii unaomba mahojiano katika kituo kimoja na heshima uwapayo hao basi igawe kwa wengine katika kipimo kile kile hapo utafanikiwa mno. (Hakika)

Ni wasanii wengi tu hata ukipanganao mahojiano hawaji na hata wakija hawaji kwa wakati, ama akagoma kabisa kukupa ushirikiano lakini ajabu akalalama juu ya mtu mmoja na kituo kimoja kuwa hakimpi mahojiano. (Jamani)

Ni wazi muziki una mengi na wasanii wenye mengi ye kusikitisha mno, msanii anakataa mahojiano huku na kule anasema hapewi, kuna vitu vinasikitisha mno. (Huzuni)

Ni vyema kubadilika kwa maana muda ni sasa maana daima mswahili husisitiza yakuwa “Saa haingoji mfalme” (Tafakari)…

#MuzikiNiSisi