‘Sio kila mazingira yakubadilishe ila badilika kulingana na mazingira’ Joh Makin Sehemu I

‘Sio kila mazingira yakubadilishe ila badilika kulingana na mazingira’ Joh Makin Sehemu I

Ukweli ni chukizo kwa wasanii wengi na mashabiki wengi wa hiphop hasa wale ambao hujiita wanaharakati, ingawa mpaka leo hatujajua harakati zao hasa ni zipi. Maana muda mwingi hutumia kukashifu maendeleo ya wasanii wengi bila kujali nguvu na muda ya msanii husika katika kuwekeza katika kazi yake.

Ni wazi kama ukitaja marapa bora waliopo chini ya mwamvuli wa hiphop wa muda wote huwezi kuacha kutaja jina la Joh Makin. Licha ya vijiwe vingi vya hiphop kuendeleza propaganda yakuwa Joh sio msanii wa hiphop kwa maana ya kutumia midundo ambayo sio ya hiphop, wakati huo huo wanasahau hiphop haina nguzo ya mdundo lakini pia nyakati zinabadilika na maboresho ya muziki kuja kwa namna pana.

Lakini katika ile kweli hata wale ambao tunawaona ni wasanii bora wa hiphop ambao wanasimamia nguzo na misingi mbona wamewahi kutumia midundo ya zamani yakina Marijani Rajabu je!ile ni midundo ya hiphop?

Muziki ni biashara pana mno, na kila msanii ameingia kwenye Sanaa kufanya kama kazi yake kuu katika kuendeleza maisha yake na familia yake.

Hivyo kumuacha msanii kufanya kile ambacho anaweza ni jambo jema Zaidi na sio kumuwekea mipaka.

Daima hupenda na tunafurahi kuzungumza ile kwenye yenye kweli maana hutufanya tuwe huru. Lakini katika kuhubiri ile kweli inasaidia kujenga mitazamo yenye chachu ya maendeleo katika muziki huu wa hiphop.

Ukitazama miaka ya 2003-2005 wakati taa ya hiphop ya Joh Makin inaanza kuwaka ni wazi aliwapa mashabiki kile watakacho kwa wakati huo. Kwa maana mazingira yalitaka kufanya wimbo kama Hao, lakini miaka ya baadae 2006-2010 nyimbo kama chochote popote, ufalme, dakika 90, muda, zamu yangu, na nyingine nyingi.

Lakini katika nyimbo zake ni wazi amekuwa na mabadiliko kuanzia tungo mpaka midundo.

Jambo hili limeendelea kumfanya kuwa bora kwa maana ya kusoma alama za nyakati katika muziki huu. Lawama ni nyingi yakuwa Joh anabebwa lakini jambo halina hata chembe ya ukweli.

Joh anabebwa lakini anabebwa na akili zake binafs ….

Itaendelea …

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa