Siku 365 za Darasa alivyopishana na fedha za mitandao na anguko la muziki wake.

Siku 365 za Darasa alivyopishana na fedha za mitandao na anguko la muziki wake.

Hakika semi ya mswahili yakuwa “Akili ni nywele na kila mtu ana zake” imetimia vyema katika uhalisi na uhalisia wa maisha ya Darasa ya muziki katika ngazi ya mtandao.

Ni mjuzi yupi wa muziki ambaye hakunena lolote juu ya ukimya wa msanii Darasa,  kuanzia ngazi ya mtandao mpaka muziki wake? Hakika hayupo. Lakini mashabiki kila leo wamekuwa wakiandika mengi kwenye posti ya mwisho ya Darasa katika mtandao wa picha ‘Instagram’ na ni  katika upana wa lalamiko.

Lakini nani anajali? Darasa? Au watu wake wa karibu? Hakika hakuna maana ana amini katika uhalisi wake autendao. (Kimya).

Leo hii Darasa anatimiza siku 365 bila kutumia mitandao ya kijamii kuanzia Facebook, Instagram, na Twitter. Na mara ya mwisho kutumia mitandao ya kijamii kwa maana ya kuweka posti ni 12.8.2017 ilihali leo ni 12.8.2018 ni ukamilisho wa siku 365 kwa maana ya mwaka 1.

Jambo hili si jema kwake kwa maana ya nyakati za sasa katika utegemeo wa mitandao katika mengi ya muziki lakini msanii kuingiza fedha kwa kuweza kuweka matangazo mengi ya kampuni tofauti.

Bila uficho ukimya huu wa mitandao ya kijamii umemnyima fedha nyingi mno, lakini pia umeongeza nguvu ya anguko lake la kimuziki. Ila wajuzi wanaamini yeye hawezi kujua maana daima “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni”.

Katika kweli yenye kweli Darasa hakupaswa kuwa kimya katika tumizi la mitandao ya kijamii, maana uhalisi ukiwa kimya kwenye ngazi ya mtandao mashabiki huacha kukufuata.

Wapo wajuzi ambao hunena yakuwa “Pengine Darasa anajipanga vyema hivyo kwa sasa hana cha kuweka kwenye mtandao”. Ni wazi cha kuweka anacho tena kwa hali ya upana.

Ikumbukwe wengi wamemjua Darasa kwenye wimbo wake wa ‘Muziki’ 2016 hivyo angekuwa ni mwenye kuweka kazi zake za zamani katika machapisho ya kueleza mengi hakika ingeleta maana kubwa.

Ila hata kuweka posti akiwa katika studio tofauti pia ingeleta tumaini jema kwa mashabiki wengi mno lakini hata kurasa zake kuendelea kuongeza kwa wafuatiliaji maana vingekuwa ni zenye uchangamfu.

Lakini katika ububu huu nani azifuate? Hakika hakuna ndiyo maana ya mgando wa wafuatiliaje ni wale wale mpaka sasa.

Kuna sababu kwa Darasa kutoka shimoni na kunena hadharani uhalisi wake ikumbukwe si lazima msanii akitoa wimbo ndiyo afanye mahojiano kama ambavyo imekuwa ni desturi sasa katika muziki wetu.

Msanii anaweza kufaya mahojiano bila kutoa kazi yoyote ile, hivyo ukimya wa Darasa ni wazi unazidi kumuangusha vyema kimuziki. Yafaa atoke na anene jambo lenye kuleta matumaini mbele ya mashabiki wake.

Na daima mswahili hakuacha kunena hadharani yakuwa “Hasara humfika mwenye mabezo” ni vyema Darasa ajitafakari tena na tena.

#TuzungumzeMuziki