Siasa inaendelea kuharibu muziki kwa mambo 3.

Siasa inaendelea kuharibu muziki kwa mambo 3.

Upepo wa siasa ni mkubwa kwa maana kila mwananchi anaongea siasa. Ni ajabu matendo ya kisiasa yamekuwa na nguvu kuliko muziki kwa sasa.

Licha ya wengi kuzungumza siasa kwa uwazi lakini si katika kuelewa kwa upana bali “Livumalo ndilo liongelewalo”.

Hakika katika nyakati fupi kwa maana ya 2015 -2018 siasa imeharibu muziki kwa upana. Ingawa wanasema siasa ni maisha lakini hili la sasa lina utatizo mkubwa katika sanaa ya muziki.

Tumeona ni vyema kuanisha mambo 3 yenye usiasa katika kuharibu muziki kwa hali nzuri. Maana yapasa tuwe wa kweli nyakati zote.

“Urafiki” hili ni jambo la kwanza ambapo wenye kufaidika ni wale wenye urafiki/ulezi na wanasiasa katika mengi. Hivyo ambao hawana urafiki hawana thamani mbele ya wenye siasa yao. (Kipaumbele)

“Zuio” Hakika kitendo cha sehemu nyingi za wazi kuwa na zuio la kupiga muziki mpaka alfajiri imepunguza vyema kutumbuiza wasanii wengi.

Maana katika kweli matamasha ya wazi hayako tena ambayo yalikuwa ni yenye kuleta ujazo wa uchumi wa msanii husika.

“Hisia” Mashabiki wana hisia yakuwa wasanii ndiyo wenye kufaidika na keki ya ulaji, hivyo mashabiki ni wenye hisia za chuki mbele ya msanii pale tu aonekanapo na mwanasiasa. Na lugha kali ndiyo hufuatia katika mitandao ya kijamii.

Lakini yote haya ni zao halisi la ‘Kujipendekeza’ Hivyo lazima wasanii wakose uhalisi wa kazi zao kwa ujumla bali mmoja mmoja maana wapo ambao hawana kasumba ya kujipendekeza. (Msimamo)

Je!muziki utasonga? ni wazi hautasonga maana muziki hausaidiwi ila anasaidiwa msanii pekee. Hakika ili tusonge yapasa muziki ndiyo usaidiwe kwa uwazi na kweli lakini kumsaidia msanii mmoja na wengine kuwa kando hakika hatuwezi kujenga.

Tafakari….!!!

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa