Si ni nani hata tusipongezi uzao wa Wasafi Tv?

Si ni nani hata tusipongezi uzao wa Wasafi Tv?

Hapana!! yafaa tuseme kwa sauti ya juu yakuwa Hongera kwa wote ambao mmehusika kuifanya Wasafi Tv kuwepo.

Na tunaona pongezi nyingi za wasanii na wadau mbalimbali, kwa hakika ni jambo jema.

Ila katika upande wa wasanii ni lazima waelewe na watambue vyema maneno ya wasafi kwa upana hasa hashtag ya #SanaaImezaliwaUpya.

Maana katika kweli yenye kweli wameanza vyema kupiga kazi za wasanii wengi zaidi katika muda mchache mno.

Na wasanii wameweza kuongea na kuandika mengi, ni vyema muweke akiba ya maneno lakini maandiko. Maana “Liandikwalo, halifutiki” Wakati “Lisemwalo, litaishi”

Wasafi Tv pia wana taratibu zao katika muendelezo wa biashara yao, hivyo wasanii wasitarajie yakuwa itakuwa hivyo kila leo. (Kupigwa nyimbo)

Kuachwa kupigwa nyimbo kwa wasanii kadhaa kutakuwepo tu, na ni pale ukienda tofauti na matakwa yao. (Uhalisi)

Ni vyema tukumbuke kumbukumbu hata wakati wa kuzaliwa kwa Efm dhanio lilikuwa kubwa mno kwa wasanii wengi yakuwa sasa watapigwa mno. (Kupatikana mwarobaini)Lakini wapi!

Maana ya kuandika haya ni kuwakumbusha wasanii yakuwa ni vyema kuishi kwa usawa na kufuata matakwa ya Media husika inataka. (Kweli)

Vinginevyo kutakuwa na malalamiko ya kila
leo, ilihali ukishindwa kuishi kwa matakwa ya Media husika, hakika lazima utaleta matata.

Lakini hatuna la kusema zaidi ya “Huwezi kuona msitu, ukiwa msituni” (Msanii)

Kujifunza kutafakari ni jambo jema na kubwa zaidi. Na pasipo maono hakuna faida hapo, kheri yule mwenye kutafakari yajayo maana ataanda kesho njema.(Amka msanii)

Na yafaa kila upande uheshimiwe ndiyo ambavyo utapata mafanikio (Msanii) (Media).

Lakini mswahili hunena yakuwa “Katikati pasikuchangaye ukasahau chanzo” (Tafakari)

#TuzungumzeMuziki

La! Hasha! pongezi kwa Wasafi Tv na watu wake wote. Tizneez tutatuma salamu zetu kwa upana zaidi pale ambapo muda utaturuhusu.

#TuzungumzeMuziki