“Si kazi rahisi kupata nafasi kwenye muziki ila ni rahisi kupotea kwenye muziki”

“Si kazi rahisi kupata nafasi kwenye muziki ila ni rahisi kupotea kwenye muziki”

Muziki umekua na tunaona kila leo ongezeko la wasanii kwa asilimia kubwa. Ilihali wasanii ambao wameweza kupata nafasi ni wengi lakini wenye kuweza kubaki katika nafasi hiyo ni wachache mno.

Ni kazi ngumu mno kwa sasa kwa msanii kupata nafasi na kuweza kukubalika na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Hii ni kutokana na uwingi wa wasanii katika uhalisia wengi ni wenye vipaji hivyo mpaka upate nafasi yapasa uwe na kitu cha ziada.

Lakini tunaona namna ya wasanii wengi hutafuta nafasi kwa ugumu lakini baada ya muda mchache kupita huanguka kirahisi. Jambo hili si jema kwetu na hatuna sababu ya kuacha kuandika walau msanii aweze kujikomboa na kikombe cha anguko.

Ni wazi wasanii wengi wakishapata nafasi hujisahau na kuanza kuishi maisha ambayo hayana  nidhamu kuanzia kwenye media mpaka kwa mashabiki.

Ni vyema msanii kuweka nidhamu mbele kwa maana nidhamu ndiyo ngao ya kila jambo ufanyalo.

Hivyo ukizingatia nidhamu ni wazi maisha ya Sanaa yako yatakuwa marefu kwa maana ya kujua namna ya kulinda vyema bidhaa yako ya Sanaa.

Bidhaa ya Sanaa ni rahisi kuchafuka na kupoteza mvuto mara tu pale msanii anaposahau yakuwa nidhamu ni ngao yake.

Kwa upana wapo wasanii wengi ambao vipaji vya ni vikubwa lakini nidhamu imeweza kuwaangusha na mashabiki kuwaona yakuwa ni wasanii wa kawaida mno.

Hivyo ni vyema kuishika nidhamu na kuitanguliza kila mahala.

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa