Shilole anapaswa kujihukumu kwa kuvunja miiko ya Sanaa.

Shilole anapaswa kujihukumu kwa kuvunja miiko ya Sanaa.

Wengi wamekuwa wakihoji ni kwanini Shilole si msanii ambaye amewahi tokea mara 2 hapa Tizneez.

Jambo ambalo mnapaswa kujua Tizneez nyakati zote huzungumza muziki tu. kwa maana ya Hivyo ni wazi hatuoni cha kuzungumza juu yake maana katika ile kweli hatuoni muziki wake bali mengi yahusuyo mahusiano na mengine yaliojaa fedheha kubwa kwa watu wengi.

Lakini kama akifanya muziki katika ile kweli ni wazi hatuwezi kufunga vinywa vyetu katika kuzungumza muziki wake. Lakini wakati sisi tukiona fedheha ni wazi inaonekana yakuwa wengi ni wapenzi wa mambo hayo.

Hivyo tunaamini kuna uwanja mkubwa wa kutazama aibu hizo ambazo kwetu hatuoni kama zinatija hata kwa udogo.

Lakini waswahili husema “Dunia huleta baya na ovu” kwa maana ya muziki umeleta wasanii na watumia/wauza miili.

Bila kificho Shilole anatumia kivuli cha muziki kufanyia ufuska. Ni wazi anapaswa kujihukumu kwa kuvunja mno miiko ya sanaa.

Lakini ndugu zetu yafaa mjue hekima za waswahili “Mwenye njaa hana miiko”

Lakini ni vyema kuthamini zaidi mwili wako,na ni jambo baya Fedha kubadilisha au kuvunja thamani ya utu wako. (Fedheha) Na hata katika maandiko muhimu zaidi yasema “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu, Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi”

Lakini imefika wakati wa kutokushangaa haya maana daima waswahili husema “Samaki huanza kuoza kichwani” (Akili)

 

Nenda Instagram @tizneez kuona ambacho amekifanya Shilole.