“Samaki huanza kuoza kichwani” Jux

“Samaki huanza kuoza kichwani” Jux

“Uzuri wa mkakaya,undani hauna kitu” Na “asiyejua maana usimwambie maana” Muziki huujabadilika ila wasanii ndiyo wamebadilika hasa katika matendo.

Lakini ndugu zetu yapasa tujue “Usipoziba ufa utajenga ukuta”
Kama leo hatukemei haya mwisho wa siku itakuwa ni kawaida kuwaona wakiwa hawana nguo kabisa.

Maana kwa upana hivi vitabu vya mzungu yani Facebook,Instagram, na Twitter bila umakini na akili hakika vitakuvua nguo.

Pichani ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Juma Jux.

Ukimuhoji mpigwa picha hii yakuwa kwanini picha yako hii imesambaa atasema “Imevujishwa na ni chukizo kwake” lakini katika upana ni nani kapiga picha hiyo? na alipiga iweje?na kwa matumizi yepi?

Ila haipasi kumlaumu mtu huyu maana “Usigombane na mkwezi,nazi imeliwa na mwezi”

Tunafikiri kuna kila sababu ya kujifunza kwa msanii kama Aslay maana bila picha mbaya wala jambo baya muziki wake umeweza kusafiri katika kila sikio la mpenda muziki.

Lakini ndugu zangu tusishangae wasanii ambao wameegemea haya mambo mabaya kwa maana “Samaki huanza kuoza kichwani” (Akili)

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez
Facebook page Tizneez
Instagram Tizneez
Youtube Tizneez
Tuachie maoni yako hapa