“Sallam Sk sio shujaa wa muziki, bali genge lake la Wcb”

“Sallam Sk sio shujaa wa muziki, bali genge lake la Wcb”

Kujifunza kutafakari ni jambo jema na zuri. Mashabiki wengi wa sasa ni watu wa kuendeshwa na hisia na sio hoja.

Wengi hupenda kulaumu na kushabikia ilimradi, na pia si watu wenye kujua historia ya muziki bali hapa ulipo.

Na shida walionayo ni moja sio watu wa kujifunza na kujua kuwa tofauti ya wasanii na Ruge haijaanza leo ni tangu na tangu kabla ya mitandao lakini baadae mitandao ila kabla ya mtandao wao pendwa Instagram.

Tumeona namna kauli ya Sallam meneja wa Diamond alivyochukua muda wao na kila mtu kutoa mawazo yake lakini mawazo yemefikishwa kwa lugha kali.(Mashabiki)

Na wengi wakiongozwa na hisia ya kuwa Sallam ni shujaa kwa kuandika jambo ndogo kama lile kuhusu Ruge *Instagram*.

Yupo msanii mmoja chipukizi aliyeshindwa kuficha hisia zake na kusema “Ruge anaharibu sana muziki Sallam alivyosema ametusaidi”

Kitu ambacho anapaswa kujua Sallam amesema kwa kuwa yeye amekaliwa shingoni kwenye tonge lake, maana ukumbuke kuna watu walishayasema haya tena kwa upana na urefu wake mwaka 2009 -2011.

Kiasi cha Serikali kuingilia kati na kutafuta suluhu kwa upande wa Ruge na Kundi zima la Vinega likiongozwa na Sugu.

Ni vyema mjue na mkumbuke Sallam hapiganii muziki bali tonge lake, hivyo kujidanganya yakuwa anasimama katika ya muziki wote ni fedheha.

Kwani wakati anakula mema ya Ruge kwa pamoja alikuwa akisema nini? zaidi ya kusifu uwepo wa Clouds Media Group. (Ni vyema kukumbuka kumbukumbu)

Ni vyema pia mjue ndugu wasanii na mashabiki yakuwa Sallam si shujaa wa muziki bali ni shujaa wa genge lao Wcb katika kusimamia ugali wao .

Kumuita shujaa wa muziki ni kuukosea muziki wenyewe na waasisi ambao kwa nguvu zao waliujenga na kuupigania wakati wote.

Hapa tunazungumzia wasanii kama Mapacha, Sugu,Mkoloni,Rama Dee, Soggy Doggy, G Solo, Ludigo, Suma G, D wa Ghetto, Swahili Original (Kinega), Danny Msimamo, Rado, na wengine wachache.

Sasa ya nini wengi wapotoshe? ni vyema kurejea historia. Ni sawa useme Lady Jaydee alipigania muziki kwa kusema mabaya ya Ruge na Clouds.

Ni wazi hapana alipigania tonge lake maana aliongea ambayo yalimshinda. Na ni vyema mashabiki mjue ukweli maana mtakuwa huru Sallam ni meneja wa Diamond sio muziki wa Bongo Fleva.

Na nyakati zote waswahili hunena yakuwa “Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu” (Shabiki) Lakini ndugu zetu yapasa mjue “Mwomba chumvi huombea chunguche”

Tafakari..!!

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment