Sallam Sk ni vyema kutumia akili kwenye mchanganuo wa hoja.

Sallam Sk ni vyema kutumia akili kwenye mchanganuo wa hoja.

Hakika mswahili hakukosea na semi yake ya “Macho hayana thamani, kama akili ina upofu”

Katika uhalisia wengi hushindwa kuishi katika akili zao, na wengi kubaki tegemezi na kuishi katika akili za watu. (Fedheha)

Ilihali yapasa watu wajue yakuwa “Ukishindwa kutumia akili yako, basi akili yako itakutumia maradufu, na hapo ndipo upumbavu wako utadhihirika” hakika waswahili ni wenye semi zenye uhalisia na kweli.

Imeshangaza mno kwa Sallam Sk ambaye inaaminika yakuwa ni meneja wa msanii mkubwa Afrika sasa ambaye ni Diamond Platnumz na Genge la WCB kuandika ujumbe wake ambao ni wazi hauna hoja kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha ‘Instagram’

Na ameandika hivi “Habari za muda huu waungwana. Tumepigiwa simu na vyombo vya habari kila sehemu kuulizwa juu ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa, nimeona tukiwa kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama WCB tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa Paul Makonda.

Ambae ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana, kwahiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima mlezi wetu azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka basi ameridhia yeye binafsi zitoke, kwahiyo sioni sababu ya nyimbo ya Hallelujah na Waka kufungiwa kama inavyosemekana maana sisi hatujapata barua ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na kwa sababu ipi.

Kama kweli zimefungiwa basi mlezi wetu ataweza kuongea mengi zaidi yangu mimi. Nawatakia Weekend njema. Pichani nipo na Babu Tale tumevaa jezi za Lipuli”

Kwa ujumbe huu inaonyesha namna ambavyo wanafanya kazi kwa kukurupuka, nyakati zote taasisi kubwa huwa kuna msemaji ambaye huwa ni Afisa Habari Mahusiano (PR) ambaye yeye huandika maandiko yenye kujitosheleza. Je!Mlezi yeye ndiye?

Andiko hili la Sallam ni wazi halitoshi na halifai kuandikiwa na mtu kama yeye ambaye inaaminika ni meneja. (Ufahamu)

Lakini kazi ya meneja ni nini hasa? Kiasi cha yeye kushindwa kutoa tamko?

Ni mangapi na mara ngapi amekuwa akitoa matamko juu ya kazi zote za msanii husika, na iweje leo asema yakuwa  Mh Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndiye atatoa tamko?

Lakini ni wazi ameshindwa kutofautisha kazi ya mlezi na kazi ya BASATA.

Ni vyema kujua pia yakuwa mlezi wao kuamua kazi hii itoke na hii isitoke hizo ni siri zao za malezi yao, wala havipaswi kuingilia kwa wajuzi na wabobezi wa maswala ya Sanaa ya Muziki.

Ila katika kweli Mh Paul Makonda anaweza asijue kuhusu makosa ya kimuziki bali makosa ya kazi yake afanyayo kila leo. (Siasa)

Maana hata waswahili wana semi yao yasema yakuwa “Ukijua upande huu, upande huu haujui”

Hivyo ni wazi Sallam ameteleza tena kiwepesi mno, mithiri ya mtu afunguapo taulo msalani.

Lakini anapaswa kujua yakuwa “Mwenye hakima daima huchunga kinywa chake katika kila neno atakalo kuwa anasema, haijalishi ni eneo gani bali kwenye kila leo ya maisha yake”

Ila “Kukosea njia, ndiyo kujua njia” ni wazi yapasa Sallam aishi maisha ya umeneja kweli na si umeneja jina.

Na waswahili hawakuacha kusema yakuwa “Kheri kujikwaa kidole, kuliko ulimi” Na “mtu mzima akivuliwa nguo hadharani, huchutama”

Tafakari….!!!

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa