Sallam Ana meneji maisha ya Diamond Platnumz au Muziki?

Sallam Ana meneji maisha ya Diamond Platnumz au Muziki?

Kuuliza si ujinga hata siku moja, Sallam ana meneji maisha ya Diamond Platnumz au muziki? Hili ni swali la mashabiki wengi mno.

Na swali hili limekuja mara baada ya Sallam kuposti picha ya Zari kuandika “Still the chosen one” Zari ni mzazi mwenzake na Diamond Platnumz ambaye mapema leo Diamond Platnumz amekubali zile habari ambazo zinaonekana zilikuwa ni shutuma za kuwa yeye ni baba wa mtoto wa pili wa Hamisa Mobetto.

Ni wazi mara nyingi imekuwa ikionekana Sallam akiingilia mambo mengi nje ya muziki wa Diamond. Jambo ambalo ni wazi linaleta maswali mengi kwa mashabiki kuwa ni meneja wa muziki au maisha ya Diamond? Kwa maana ni wazi Diamond ana maisha mengine nje ya muziki.

Ni wazi Sallam bila umakini wa matendo afanyayo mara kwa mara katika mitandao ya kijamii ni wazi yanashusha thamani yake ya kuonekana meneja bali kuonekana ni mpambe.

Lakini ni vyema mjue “Uficho wa siri ya mapenzi ni ugumu kwa mtu yoyote kuchaguliwa mpenzi” Hivyo ni vyema Sallam kubaki kumeneji muziki na asiingilie maisha ya Diamond nje ya muziki.

Pia sio kila jambo liwe katika mitandao ya kijamii, ni vyema kujifunza Zaidi kwa meneja wengine nje ya Tanzania, wakati wote huzungumza muziki wa msanii wake na si jambo jingine #TuzungumzeMuziki

Ni ngumu kuona meneja wa msanii kuandika andika hovyo katika mitandao ya kijamii kwa maana meneja humuongoza msanii kwenye mambo yaliyomema na faida.

Umakini unahitajika kwa vijana hawa kwa maana “Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake”

Ni vyema Sallam kutazama hatua kabla hazijaja siku za kuonekana ya mpambe mwema.

Lakini ndugu zetu yapasa mjue “Fahari mama wa ujinga”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa