Sababu tatu za wimbo wa Darasa ‘Muziki kufanya vizuri 2016-2017.

Sababu tatu za wimbo wa Darasa ‘Muziki kufanya vizuri 2016-2017.
Kulikuwepo kwa nyimbo nyingi katika kiwanda cha bongo fleva/hiphop katika mwaka 2016 mpaka mwaka huu 2017.
Kila msanii ametoa kazi nzuri na bora kwa nafasi yake, maana ni wazi ushindani umekuwa mkubwa mno. Hivyo kila mmoja hujitahidi kufanya kilicho bora zaidi.
Darasa anabaki kuwa msanii kinara aliyefunga mwaka 2016 vyema, na msanii ambaye amefunga mwaka 2017 vyema zaidi, na wengi husema ‘muziki’ ni wimbo wa taifa. Lakini kabla ya kutoka kwa wimbo wa muziki Darasa alikuwa na wimbo kama Too Much,na Utanipenda ambazo pia ziliweza kufanya vyema mwaka 2016
‘Muziki’ni wimbo wake ambao umefanya hata wasio wapenzi wa muziki wa kizazi kipya walifahamu jina la Darasa.
Darasa anasimama kama rapa aliyooko chini ya kivuli cha hiphop. Maswali ni mengi juu ya wimbo huu wa ‘muziki’ kufanya vizuri zaidi kuliko nyimbo nyingine yoyote mwaka 2016.
Kwanza kabisa Darasa alijua mashabiki wanataka nini, kuna wasanii wengi wazuri lakini kosa wafanyalo ni kutokujua mashabiki wanachohitaji. Ni wazi mazoea yanaangusha wasanii wengi badala ya kuwainua, mashabiki wa sasa wanapenda vitu vyepesi zaidi.
Ikumbukwe Darasa huyu wa wimbo wa ‘muziki’ ndiyo yule yule wa Sikati tamaa, Weka ngoma, Nishike mkono,Tunaishi, Mikono juu, Kitabu na nyingine nyingi. Darasa alijua mashabiki wanataka kucheza na kusikia mashairi ‘maneno” mepesi yenye kushikika haraka, na jambo hili liliweza kufanikiwa kwa siku ya kwanza tu tangu kutoka kwa wimbo huo kila shabiki aliweza kushika mashairi hivyo kufanya wimbo kuweza kupenya zaidi.
Kuwepo kila Media, hapa ndipo ambapo tunaona maanguko ya wasanii wengi na huwa wanakuwa na kazi nzuri. Ni wazi wapo wasanii ambao unajua kabisa kuwa msani huyu ni Radio Fulani, na hata toa ushirikiano na vituo vingine au hata kama akitoa basi ni kwa asilimia ndogo.
Darasa alikuwa kila media katika kutangaza wimbo wake huu wa ‘muziki’. Utofauti wa Darasa ni katika blog na media za mikoani, ni wazi Darasa alizipa nafasi ambayo alizipa zile media ambazo tunaamini ni kubwa. Kufanya mahojiano na kila mwanahabari ambaye alihitaji kujua lolote kuhusu wimbo huo, bila kujali yupo media gani.
Nguvu ya mtandao, Wakati wasanii wakiwa wemejikita kupiga picha binafsi na kuziedit kupata mng’aro, Darasa alikuwa akichukua video fupi fupi kwaajili ya kuonyesha mapokeo ya wimbo wake katika kila eneo ambalo alikuwa anapita.
Ni wazi video zile zimechangia kuamsha hisia za mashabiki wengine ambao wako mbali na eneo husika.
Darasa alijua jinsi ya kwenda na wakati hasa katika mitandao ya kijamii, hakuwa mtu wa malalamiko zaidi ya kuposti mapokeo wimbo kila wakati. Darasa pia alitumia vyema mtandao kuonyesha mabadiliko ya matumbuizo yake hasa wimbo wake wa ‘muziki’
Sina shaka na uwezo wa Darasa na sina shaka juu ya kushuka kimuziki. Maana hata kupitia kinywa chake aliwahi kusema “Sipagawi na ustaa wakati mifano ipo wazi, wangapi walitamba na leo wamemwaga radhi”
Nategemea kumuona Darasa mpya kila siku kwa kufanya mambo haya matatu kila anapotoa wimbo na pia kubadilika kulingana na mazingira. Hivyo yaweza kuwa zaidi ya haya matatu.
Follow Twitter Tizneez
Facebook page Tizneez
Instagram Tizneez
Tuachie maoni yako hapa

Attachment