Sababu kuu za Nikki Mbishi kutopewa nafasi na Media kubwa

Sababu kuu za Nikki Mbishi kutopewa nafasi na Media kubwa.

Ukijua ukweli na ukikaa nao kifuani hakika ni wazi hauna maana.

Mashabiki wengi na baadhi ya wasanii humuona Nikki Mbishi ni msanii mwenye kulalama na sio kazi.

Katika kweli yenye uhakika Nikki Mbishi ni moja ya wasanii wenye kazi nyingi zaidi, na nyingi tayari zipo katika mtandao lakini nyingine ndani.

Hivyo ambaye anaona Nikki Mbishi hana kazi nyingi ni wazi ni wale ambao hawafuatilii muziki wake kiundani.

Na wala hatupaswi kulaumu watu hawa bali tuseme kweli juu ya Media zetu kubwa maana katika kweli ndiyo huaminika katika maaminisho yote juu ya sanaa ya msanii husika.

Tukisema kweli yenye kweli ni wazi katika usawa wa Nikki Mbishi kwenye nyakati hizi hakuna mchanaji yoyote yule ambaye anafikia hata usawa nusu ya Nikki Mbishi. (Uhalisia)

Ila sikio la wengi lipo katika Media kubwa hivyo maaminisho yao yanafanya mashabiki waamini yakuwa “Wasikikao/Waonekanao Radio/Runinga ndiyo bora” (Uongo)

Sasa ya nini nasi tuishi katika uongo huo? hapana hatuko tayari.

Hivyo ili kuwa nje kundi la wahubiri uongo ni vyema tuseme kweli yenye kweli juu ya mambo makuu ambayo ndiyo chanzo hasa cha Nikki Mbishi kutopewa nafasi na Media kubwa.

“Kunyenyekea” Tatizo linaanzia hapa maana katika kweli watu wa Media kubwa wanataka kunyeyekewa kupita kiasi.

Sio watu wenye kujali kazi bora ya msanii bali kunyenyekea zaidi. Na hapa tunapenda mtofautishe kati ya nidhamu na kunyenyekea (Hofu).

Kama wanahubiri Nikki Mbishi hana nidhamu je!wameshamuita kwenye mahojiano na hakuenda? au amekataa kabisa kupokea hata simu? au wapi, lini na nani hakupewa ushirikiano na Nikki Mbishi (Katika kazi)

Na ni mara ngapi Nikki Mbishi huwapigia simu na kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno watu wa Media kubwa, je!wanamjibu? ni wazi hukaa kimya nyakati zote na baadaye husema hana nidhamu, hivi nidhamu gani wanataka? ni wazi hakuna zaidi ya kunyenyekea.

Hivyo kwa mashabiki wenye hisia juu ya nidhamu ya Nikki Mbishi sisi twasema nidhamu ya kazi anayo tena kwa ukubwa, na pia tutofautishe maisha yake ya sanaa na maisha yake mengine ya nje ya sanaa. (Mtandao, Mtandao)

Huenda mkadhani yakuwa tunaandika kwa hisia, hapana hapana huu ni uhalisia.

Tunasema haya maana tunayajua na tupo nao kila siku. Ni wazi watu wa Media kubwa kuanzia Dj na Mtangazaji ni wenye kutaka mno habari kuitwa bro/sister lakini msanii awe chini yake zaidi nae ndiyo awe juu. (Fedheha)

Na hawajui maana ya heshima/nidhamu bali wao kutaka kunyenyekewa zaidi.

Yani kama msanii tu hajaposti tangazo la kipindi chake au hajaposti lolote juu ya mfanano wa tarehe ya kuzaliwa kwake pia huwa ni tatizo. (Soni)

Hakika huu ni ujinga ulioje, maana mchanganyo wa kazi na maisha binafsi ni mkubwa katika muziki wa Nikki Mbishi.

Lakini ndugu zetu mashabiki mnapaswa mjue yakuwa watu wa Media pia wanataka zaidi msanii ajipendekeze zaidi.

Na nyakati zote ni wazi “Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake”

Itaendelea……

#TuzungumzeMuziki