Sababu 3 za wimbo ‘Seduce me’ wa Ali Kiba kufanya vizuri kuliko waimbaji wengine.

Sababu 3 za wimbo ‘Seduce me’ wa Ali Kiba kufanya vizuri kuliko waimbaji wengine.

“Apigaye ukuta ngumu huumiza mkonowe” Nguvu ya ubishi bila hoja ni kubwa, ilihali wabishaji hawafikiri nguvu watumiayo kubishana na ukweli. Na wamekuwa wepesi kusahau “ubishi mwingi huvuta matata”

Ni wazi ubishi wao umekuwa ukileta matata mengi katika mitandao ya kijamii lakini hata katika vijiwe vingi vya muziki wa kizazi kipya.

“Taratibu ndiyo mwendo” Team Tizneez huwa hatuna haraka ya kutoa hoja wala kuandika maandiko ili kutafakari kwa muda mzuri na hii ni katika kuweka na kutaka mambo yaende sawa.

Kila mtu amekuwa akishangazwa na jinsi wimbo Seduce Me wa Ali Kiba kufanya vizuri katika muda mfupi tofauti na waimbaji wengi kwenye nyakati hizi.

Ni wazi kuna mambo matatu ambayo yamefanya wimbo huu kufanya vizuri katika muda mfupi.

Bila Kiki, ni wazi hakukuwa na kiki ya aina yoyote katika utoaji wimbo huu. Imekuwa ni kawaida na mila sasa kwa wasanii wengi waimbaji kabla ya kutoa wimbo hufanya kiki ili tu kuzungumziwa Zaidi. Kiba alitoa wimbo huu bila kiki yoyote ile, hivyo waimbaji wengi wanapaswa wajue bila kiki muziki inawezekana #ZimaKikiWashaMuziki.

Upekee, jamii ya sasa ya muziki inaamini Zaidi katika msanii kufanya kazi na msanii wa nje ndiyo afanye vyema. Lakini katika uhalisia si kweli, kazi yako ukiifanya kwa ubora ni wazi dunia itakujua. Mfano wa jambo hili ni Khalid na wimbo wake wa Aisha dunia ilimjua bila kufanya kazi na mtu yoyote yule. Hivyo wakati watu wakitarajia lazima iwe kolabo ya Kiba na Fulani Kiba akaja kipeke na upekee Zaidi.

Kubaki na uhalisia wa bongo fleva. Wakati wengi waimbaji wakikimbilia kuimba  ladha ya Nigeria Kiba akabaki na ubongo fleva wake, na katika ile kweli “Mcheza kwao hutunzwa”

#ZimaKikiWashaMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa