Sababu 2 za mtayarishaji wa Man Water kufanya kazi bora nyakati zote.

Sababu 2 za mtayarishaji wa Man Water kufanya kazi bora nyakati zote.

Muziki ni sanaa ambayo huanza kwa hisia za ndani za msanii husika ndiyo tokeo la uzao wa wimbo kuja, lakini chanzo kikuu cha muziki ni ‘hisia’Lakini muziki haukamiliki kama hakuna mapigo yenye unogesho kutoka kwa mtayarishaji, ambapo kupitia mdundo msanii huingiza sauti yenye mashairi hatimaye wimbo kukamilika.

Katika nyakati hizi watayarishaji wengi wamekosa kufanya kazi zenye kukaa nyakati zote, bali maanguko ya wimbo katika muda mfupi mno.

Lakini kwa mtayarishaji Man Water ni tofauti kabisa, nyakati zote tangu kufahamika kwake miaka 2003 ni mwenye kutoa kazi zenye kudumi nyakati zote.

Na anguko la muda mfupi kwa nyimbo nyingi za sasa kutoka kwa watayarishaji wengi chanzo chake ni watayarishaji wengi kutofuata hisia zao, bali kusimamia zaidi hisia za watu zaidi (Muigo).

Lakini pia kufuata upepo uvumavyo hakika kwa wajuzi wa muziki ni anguko pili.Lakini tofauti hizo mbili zinafanya Man Water kuweza kufanya kazi bora kwa sasa zenye kuishi nyakati zote.

Mosi, Kutofuata upepo, Man Water anajua maana ya muziki hivyo hafuati upepo uvumao, bali kuheshimu kile ambacho amebuni kwa nyakati hizo. Wakati watayarishaji wengi wakipepea na kasi ya upepo mara Nigeria au Afrika ya Kusini yeye Water anasimama katika ubunifu wake.

Na ubunifu wake unamfanya kuwa mwenye kutoa kazi bora nyakati zote maana ‘hisia’ zake ni bora kuliko muigo.

Pili, uwezo wa kutayarisha nyimbo nyingi tofauti, uwezo huu unampa heko kubwa ya ubunifu katika changanyo la kupata ladha yenye muziki tofauti kile wengi walichozoea kusikia.

Mfano hai na halisi ni wimbo mpya wa Mvumo wa radi kutoka kwa Ali Kiba. Hakika umekuja kipekee zaidi, hauna ladha ya kufanana na muziki ulioko sasa.

Ni wazi ili uwe bora katika sanaa ni vyema kusimamia na kuheshimu hisia zako, sio kufuata za watu wengi.

Kwa namna ya uhalisia wa Man Water hakika ataendelea kubaki bora nyakati zote.Na mswahili hunena yakuwa “Kuelewa pia ni kipaji”

#TuzungumzeMuziki