Rostam na Stereo katika utofauti wa ujuzi wa muziki na biashara ya muziki.

 

Rostam na Stereo katika utofauti wa ujuzi wa muziki na biashara ya muziki.

Kosoa ya Stereo kwenda kwa Rostam ni kubwa mno kila itwaapo leo, tena hukosoa kwa uwazi bila uficho.

Ni wazi Stereo haamini kabisa katika uwezo wa Rostam kwa maana ya Roma Mkatoliki na Stamina. Ambapo moja ya kauli aliyonena Stereo ni yakuwa “Uwezo wa Rostam ni mdogo sana”.

Ambapo aliongeza kwa kunena“Mtu yoyote ambaye anajua rap kweli akikaa Rostam na Ukimsikiliza Nikki Mbishi, One the Incredible, Songa, na Stereo kweli utawaona wapi Roma na Stamina?

Jambo hili limeleta ukakasi kwa wajuzi wa muziki na biashara. Ambapo tazamo kuu ni utofauti wa ujuzi wa muziki na biashara ya muziki.

Nyakati Stereo akiendelea kupayuka na kuhubiri juu ya ubovu wa Rostam lakini biashara iko kwa upande wa Rostam tena kwa upana wao.

Ujuzi wa muziki ni kitu mosi lakini kufanya biashara jambo pili. Hivyo ipo tofauti ambayo Stereo huenda ameshindwa kujua ndiyo sababu ya kunena hovyo kila kukicha kwa upande wa Rostam.

Ni shabiki yupi umwambie yakuwa Rostam uwezo wao ni mdogo na akuelewe? Hakika hayupo maana katika sikio lake huwasikia na kuwaona Rostam kila siku iendavyo.

Katika linganisho la Stereo kwa upande wa Rostam na mtu kama Nikki Mbishi, One, Songa na Stereo haliwezi kuwa na nguvu mbele ya mashabiki wengi bali wajuzi wachache mno.

Je!biashara ipo kwa wajuzi au mashabiki? Daima inabaki kwa mashabiki kwa uwingi wao, hivyo ni vyema Stereo kufanya kazi kwa upana sio kuwa mchambuzi wa muziki katika chambuo za aina ya vijembe.

Na tunaamini Stereo ni muumini wa semi ya “Vitendo dhidi ya maneno” basi kazi na zifanyike ubishani uwe ni katika soko si nje ya soko na muziki kwa ujumla.

#TuzungumzeMuziki