Rosa Ree na maisha tofauti ya sanaa na wasanii wenzake

Rosa Ree na maisha tofauti ya sanaa na wasanii wenzake.

Daima “Mazoea ni kama sheria nyakati zote”. Na uhalisi ni wengi kuishi katika uisho wa wengi katika zoeo la kila leo.

Sister P, Raha P, Zay B, Chiku K na wengine kadhaa katika kuchipuka na kustawi kwa muziki tuliwashuhudia wakifanya yao kwa upana wao.

Na daima “Shahidi ndiye mwenye neno” Na tumeona/tunaona endelezo jema la muziki wa rap kwa upande wa kike, ila changamoto bado ni nyingi.

Ingawaje kwa sasa ni kama yuko Rose Ree yu pekee kwa maana ya kukosa mpinzani katika namna ya ufanyaji wa muziki.

Kwani yupo ambaye anaweza kufikia hata robo ya Rosa Ree kwa sasa? katika upana wa biashara ya muziki na ufanyaji wake?

Daima twanena yakuwa ‘Kuchana/kuimba ni kitu mosi, pili ni namna ya kufanya biashara. Na biashara haipaswi iwe mazoea bali kwenda na uhalisi wa kulishika soko.

Na ikumbukwe wasanii wengi wa kike katika upana wao walikuwa ni wenye kuvaa kiume, lakini licha ya kiume ila hovyo kabisa.

Kiubuka kwa Rose Ree hakukuwa kuvaa kiume bali kike yenye kuvutia kwa kila mmoja mbele ya uono wa macho yake. Na daima biashara ni kuitengeneza katika uonekano mzuri.

Wajuzi wanamuona Rosa Ree katika upana wa sanaa yenye mapana. One Way imeonyesha upande pili wake ambapo ni kama ameimba lakini mitambao mizuri yenye uzuri wa kusikilizika.

Mabadiliko ya mitambao yenye ladha tofauti ni changamoto kwa wasanii karibu wote kike. Na anguko huwafika mapema mno na ni kutokana kuwa na ladha mosi yenye kukera.

Ila kwa Rosa Ree imekuwa tofauti katika hali ya ujuzi wa kujua nyakati za muziki katika badiliko lenye kuweza kumjenga na kubaki na uhalisi wake.

Lakini namna ambavyo anatangaza kazi zake katika ngazi ya mtandao ni jambo la kusifu. Ukitazama wasanii wa rap wa kike wengi wao sio wepesi katika utangazaji wa kazi zao.

Tegemeo letu ni kubwa katika yeye lakini ni kama hatolewa sifa na kuuvaa ufahari wa ubora. Maana hata waswahili wanena yakuwa “Fahari mama wa ujinga”

Hivyo fahari ikimvaa ataanguka mapema mno, vivyo basi ashike sanaa yake katika upana wa nidhamu ya kazi na hakika endelezo jema litamfika vyema.

#TuzungumzeMuziki