Rosa Ree amewezaje kufanikiwa tena bila Nahreel?


Mara chache mno msanii akiachana na mtayarishaji aliyeweza kumtoa kimuziki kuendelea mbele.

Mifano hai katika kweli ya wasanii ambao waliachana na watayarishaji wao na kupotea ni kama Mabeste, Mrap, Gosby, na Deddy.

Na hapa tunazungumzia nyakati njema za B Hitz Music Group yani Pancho Latino na Hermy B.

Na tuliona vyema kuibuka kwa Rosa Ree miaka miwili nyuma akiwa chini ya The Industry (Navy Kenzo, (Aika na Nahreel). Na mwanzoni kabisa mwa 2018 Rosa Ree aliweka wazi kuondoka chini ya The Industry, na dhanio la wengi ni kupotea kimuziki kwa maana ya historia isemavyo.

Lakini imekuwa tofauti zaidi mara tu alipoachia wimbo wa Dow. Na wengi wakasema ni bahatisho hivyo zijazo ni anguko hasa kwa upande wa watayarishaji.

Sasa hivi ni Marathon akiwa na Bill Nass hakika ameonyesha ukubwa alionao katika midondoko, lakini uandishi wenye aina ya wateja wake.

Ni wazi Rosa Ree amejua yupi ni mwenye kufaa katika upande wake wa kuandaa wimbo, ni wazi sio kila mtayarishaji atakuwa sawa mbele ya msanii fulani.

Pia jambo jema ambalo anapaswa msanii kuwa nalo ni katika kujua namna ya kuchagua mdundo.

Lakini tusishangae @rosa_ree kusonga vyema sasa tukumbuke alipita katika mikono salama ya Aika na Nahreel yenye kujua vyema maana ya biashara ya muziki lakini ujuzi wa uchaguzi wa mdundo ni njia kuu.

Ni wazi kwa sasa Rose Ree ndiye msanii wa hiphop kike aliyeshika namba 1 katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

#TuzungumzeMuziki