Rich Mavoko ni mfano wa chemchem isiyokauka katika tungo na uimbaji.

Rich Mavoko ni mfano wa chemchem isiyokauka katika tungo na uimbaji.

Tega sikio lako na usikie usikivu wa sauti mpya ya muziki, ni vyema kuondoa hisia mbaya kama unahitaji kupata uzuri wa usikivu mzuri wa sauti mpya katika sikio lako.

Daima sisi huamini katika hekima ya mswahili yakuwa “Wote wakiwa upande wa kulia na ukabaki kushoto pekee hakika watakuona” (Uhalisi)

Huu ni uhalisia wa ‘Ndegele’ ambao ni wimbo wa Rich Mavoko uliotoka katika saa chache zilizopita.

Ikiwa wimbi la wasanii wengi liko katika upana wa muigo wa ladha za Nigeria Rich amebaki na uhalisi wa bongo fleva.

Ambapo ni wazi iko na usawa wa usawia katika ladha tamu ya masikio mfano wa pepo tamu za fukwe nyakati za jioni pembezoni mwa bahari ya hindi.

Mdundo wenye mlio mithili ya malimba kutoka kwenye viganja vya Aby Dady umeleta chachu tamu ya kamilisho la wimbo mzuri wa ‘Ndegele’.

Mipito ya Rich Mavoko katika upana wa kupanda na kushuka umeleta kamilisho la muziki juu ya mlalo mzuri kwenye mdundo wa Aby Dady.

Na uzuri wa Rich Mavoko ni msanii ambaye anauwezo wa kufanya kazi katika mdundo wowote na kuendelea kubaki na ubora wake.

‘Ndegele’ ni mfano halisi wa Rich Mavoko yakuwa ni upana wa chemchem isiyokauka katika uimbaji na tungo.

Inaweza kuwa shangazo kwa ambaye hajaelewa wimbo huu, lakini mnadhani kuna haja ya kuwashangaa?. Hapana maana “Hata kuelewa pia ni kipaji”

Na tufurahie ‘Ndegele’ katika upana wa burudani ya muziki mzuri wenye ladha tofauti na zilizopo.

#TuzungumzeMuziki