Rich Mavoko na kilevi cha sifa pekee kisicho na uhalisia.

Rich Mavoko na kilevi cha sifa pekee kisicho na uhalisia.

Mpe sifa awe rafiki yako na ‘coment’ nyingi za shukurani ziwe katika ukurasa wako. Mpe kweli yenye kweli iwe chukizo na ‘block’ iwe juu yako. (Fedheha)

Imekuwa rahisi mno kwa msanii Rich Mavoko kuiblock Tizneez katika mtandao wa picha Instagram. Na chanzo kikuu ni katika maandiko mengi yenye kueeleza uhalisi wa muziki wake sasa. (Makala)

Na haswa ni upana wa endelezo lake mara baada ya kutoka WCB. Mara alipotoka Wcb amekuwa ni msanii mwenye kusuasua vyema. Na ukweli ni kwamba ni namna amekosa usimamizi hodari wa kazi zake. (Kweli)

Na maandiko ya Tizneez yalilenga upana wa nini afanye katika endelezo jema, maana ingekuwa ajabu kubwa kunena Rich Mavoko ameendelea kupiga hatua mara baada ya kutoka WCB ilihali si kweli. (Kunafikia)

Ambapo mapokeo yake katika maandiko ya kumjenga imekuwa kinyume kiasi cha kuamua kublock kabisa Tizneez. Hii haitupi shida kwa maana tunajua uhalisi wa wasanii wengi ni katika kupenda sifu ya uongo si kweli. (Uhalisia)

Lakini kimsingi wala hakupaswa kublock Tizneez bali kuchukua kweli katika njia ya kujifunza na kuendelea vyema. Ila kama anataka kilevi cha sifa pekee kisicho na uhalisia ni wazi hakina maana. (Ujinga)

Bali anapaswa apende kweli katika kujifunza na kujipanga vyema, lakini hatushangazwi na maamuzi yake kwa maana twajua yakuwa “Ili uwe na akili lazima akili uwe nayo”. (Ufahamu)

Na mpaka sasa Rich Mavako anakuwa ni msanii wa tatu katika kuiblock Tizneez, ambapo wa kwanza ni Young Killler, pili ni Motra The Future na Rich Mavoko. Na wote hawa ni katika zile kweli chungu zenye kufunza na ikawa chukizo kwao. (Doh)

Lakini hii haitoi maana ya Tizneez kuacha kuzungumza kazi zao tutaendelea kuzungumza kwa upana wa kukosoa na kusifia kwa maana kosoa na sifia ndiyo huleta endelezo kubwa la muziki. (Hakika)

#MuzikiNiSisi