Rich Mavoko kaa kitako na utafakari kabla ya endelezo la muziki wako.

Rich Mavoko kaa kitako na utafakari kabla ya endelezo la muziki wako.

Waswahili hunena yakuwa “Mwenye pupa hadiliki kula tamu”, Naam! huu ni uhalisi wenye uhalisia wa uisho wa Rich Mavoko katika nyakati hizi.

Ni wazi ni mwenye pupa katika kwenda mbio na kasi ya utoaji wimbo kwa sasa. Jambo ambalo ni wazi litamfanya aaendelee kuwa na mkwamo bila kuwa na tafakari. (Amekwama)

‘Ndegele’ ni wimbo mosi kutoa mara baada ya seke seke lake na Wcb, ambapo mpaka leo hii ni tamthilia isiyojulikana juu ya endelezo lake la kati wala mwisho. (Uhalisi)

Ingawaje Rich Mavoko amekuwa na muendelezo wa utoaji wimbo mwingine wa ‘Hongera’ na kama kawaida ameachia katika ngazi ya mtandao.

Lakini Je!mtandao pekee tena wa ‘Instagram’ unatosha kufanya Rich Mavoko aendelee kusimama kimuziki?. (Tafakari)

Ni wazi hautoshi bali uiongilio wa nguvu ya Media kama ambavyo ilikuwa awali yake. Ni nani mshauri wa Rich Mavoko sasa? Ni Dokii? Hakika kama ndiye basi atampa anguko jema. (Kweli).

Ni vyema akae kitako na tafakari pana iwe juu yake, ambapo ya kwanza ni kujenga mahusiano na vituo vingine vya radio na runinga ambavyo vilikuwa havipigi vyimbo za Wcb. Ambapo na yeye alikuwa katika mkumbo huo, na hata leo bado wamezima. (Uhalisia)

Katika kweli yenye kweli Rich Mavoko mnamsikia/mnamuona katika kituo kipi cha Radio na Runinga?. Ikumbukwe nyakati za kabla ya seke seke na Wcb alikuwa akipewa muda mwema zaidi Wasafi Tv je!hali ikoje kwa sasa?. Anapewa muda? (Hapana).

Na vituo vingine Je! anapewa muda? Hakika hana apewao zaidi ya kubaki fedheha juu yake katika njia panda na asijue aendeko. (Soni).

Njia apasayo kwenda kwa sasa ni namna ya kurudisha mahusiano yake ya awali na Media zote kama msanii ambaye amekimbia kivuli cha Wcb.

Vinginevyo atabaki kuwa msanii wa ‘Instagram’ kitu ambacho kitampa mfadhaiko na uzao wa mengi yenye mabaya juu yake.

Utoaji wa nyimbo bila nguvu ya Media kwa upande wake si njia sahihi, ni vyema ashike ushauri wa wajuzi na si kushauri washauri wenye ujuzi wa biashara ya muziki.

Ni wazi Rich Mavoko ni bora lakini kuwa bora ni jambo mosi, pili ni upana wa kuifanya biashara. Na mswahili hunena yakuwa “Hasara humfika mwenye mabezo” Tafakari….

 

#TuzungumzeMuziki