Rich Mavako baada ya kutoka Wcb amesonga mbele au amerudi nyuma? (Ulizo)

Rich Mavako baada ya kutoka Wcb amesonga mbele au amerudi nyuma? (Ulizo)

Wengi hili ni swali kuu ambalo wamekuwa wakijiuliza vyema kuhusu msanii Rich Mavako mwenye uhodari wa kutunga na kuimba kwa uzuri muziki huu wa bongo fleva. (Uimbaji)

Ni 2018 ambapo Rich Mavako aliona anapaswa kuwa nje ya Record label ya Wcb ambayo iko chini ya msanii Daimond Platnumz. Na rasmi Rich alijiunga na Wcb mwaka 2016. (Kumbukumbu)

Lakini wakati akijiunga na Wcb Rich tayari alikuwa ni msanii mkubwa mwenye mashabiki kamili. Ambapo nyimbo zake kama Pacha wangu, One Time, Silali, Uzuri wako na nyingine nyingi zimeweza kumpa heshima vyema. (Muziki)

Mara baada ya vuta ni nikuvute na kufanikiwa kujitoa Wcb msanii Rich Mavako ameweza kutoa nyimbo takribani tano. Ambapo hapa tunazungumzia wimbo kama Wazele, Ndegele, Navumilia, Naogopa, na Hongera. (Ukamili)

Lakini uhalisi ni kwamba hazikuweza kushika kama ambavyo ilikuwa awali yake kabla ya Wcb na mara ya kujiunga na Wcb. Kimsingi kwa sasa ni msanii mwenye anguko kwa maana hayuko katika mzunguko wa soko la muziki. (Kabisa)

Kwa mantiki hii inaonyesha uwazi yakuwa mara baada ya kujitoa Wcb amerudi nyuma mno. Hakuna hatua aliyopiga maana hata upana wa shoo umepungua kwa kiasi kikubwa mno. (Sikitiko)

Lakini upana wa kuamka ni mkubwa kwa Rich kwa kuwa ni msanii mwenye ujazo imara wa uimbaji na utunzi. Vivyo atakiwacho ni msimamizi hodari ajueye upana wa soko la muziki na fitina zake katika mauzo. (Kiongozi)

Ikumbukwe ‘Kufanya muziki ni jambo mosi, pili ni upana wa biashara kamili ya muziki’. Daima mswahili haachi kutujuza yakuwa “Ukitaka nyumba njema, sharti utie msingi mwema”.(Tafakari..)

#MuzikiNiSisi