Ray Vanny Ataweza kuhimili vishindo vya Nikki Mbishi?

Ray Vanny Ataweza kuhimili vishindo vya Nikki Mbishi?

Ray Vanny ni msanii kutoka Label ya Wcb ambayo inamilikiwa na msanii Diamond Platnumz.

Ray Vanny ni moja kati ya wasanii wachanga ambao wanafanya vyema kwa sasa kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya hasa bongo fleva.

Licha ya zamani kuwa ni moja kati ya wasanii ambao tulitegemea watakuwa zao bora la baadae katika muziki wa hiphop, lakini mapema tu aliamua kuwa muimbaji.

Na amekuwa akijaribu kufanya mara chache muziki wa rap ambapo tumeona aliweza kurudia wimbo wa Mr II Sugu ambao unaitwa Sugu.

Tumeona sasa kuna wimbo mwingine ambao amerap na ameachia katika ngazi ya mtandao ambao amezungumza mengi hasa kuhusu wasanii wengi. Moja ya wasanii ambao wametajwa ni Nikki Mbishi.

Ray Vanny amemtaja Nikki Mbishi katika wimbo huo ambapo amechana “Ni tofauti na Nikki Mbishi mandevu roporopo kila kitu anajifanya mwerevu”

Kupitia mtandao wa picha Instagram Nikki Mbishi aliweka kipande cha sauti ya Ray Vanny ambacho ameimba na kuandika “Umetisha sana mdogo wangu Ray Vanny nah ii Nikki Mbishi Mandevu roporopo, hapo sifanyi hata hizo interview zenu naitwa roporopo pata picha daily ningekuwa kwenye radio na tv kama Wakazi Music sijui ungesemaje maana nina madini ambayo maboss wako waliokutoa kwenu Mwakaleli wanayaheshimu.

Get what yours and respect the gods of this saga little hommie I ain’t impressed with yours short music carrier anyways”.

Je!katika swala la Ray Vanny kutupa vijimbe kwa Nikki Mbishi ataweza kupambana na Nikki Mbishi katika hili? Kwa maana ya Nikki Mbishi ni moja ya wasanii ambao ni wapesi na wazuri katika kuandika (DissTrack).

Mashabiki wanapaswa wakumbuke yakuwa hata Nay wa Mitego pale ambapo alijaribu kusema mambo kadhaa juu ya Nikki Mbishi aliweza kuandikiwa wimbo mmoja tu wa Neema wa Mitengo na hapo Nay hakuweza kusema jambo lolote tena.

Na hii ilitokana na namna ya Nikki Mbishi alivyoweza kucheza na maneno katika wimbo huo ulifanya mpinzani Nay kukosa cha kuimba tena.

Je!vipi kwa kijana mdogo Ray ataweza kuhimili vishindo vya Nikki Mbishi?

Tupe maoni yako.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa