Rama Dee maana halisi ya msanii ambaye yapasa wasanii wengi wajifunze kwake.

Rama Dee maana halisi ya msanii ambaye yapasa wasanii wengi wajifunze kwake.

#TuzungumzeMuziki ni moja kati ya maneno ambayo tumeyapa kipaumbele Zaidi hapa Tizneez. Lakini nyakati zote tumekuwa tukisema #ZimaKikiWashaMuziki.

Ingawa tupo katika kizazi ambacho hakijui wala hakithamini muziki pekee bali udaku na kiki ndiyo huwa kipaumbele Zaidi katika maisha yao ya kila leo.

Licha ya vurugu zote za kiki lakini Rama Dee bado anaendelea kuonakena kuwa ni bora katika wengi wenye majina makubwa ambayo majina yao si ya kimuziki kwa maana ya Sanaa bali kiki ambazo huwapandisha haraka na kushuka upesi kama mzunguko wa ringi lishukapo kwenye mteremko.

Rama Dee tangu kufahamika miaka 9 nyuma amendelea kupanda kila leo huku akibaki kuwa bora katika muziki wa Rnb Tanzania. Ni wazi ni ngumu kwa msanii kama huyu kushuka kwa maana ya nidhamu katika Sanaa yake.

Protocol ni wimbo wake mpya sasa ambao ni wazi umezidi kudhihilisha yakuwa Rama Dee ni mfalme wa muziki huu wa Rnb katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Licha ya kuwa na ukubwa wa kipaji lakini daima husimama katika upande mmoja wa muziki  wake tu, huwezi kusikia Rama Dee kafanya jambo baya ilimradi apate muda wa kuzungumziwa ila wakati wote watu huzungumza kuhusu muziki wake tu.

Jambo hili ni zuri na daima tunaamini atafika mbali Zaidi kwani mar azote “Hisani haiozi”

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa