Q chief unauza ng’ombe unanua bakora (Chekesho

Q chief unauza ng’ombe unanua bakora (Chekesho)

Tulikuwa ni watu wa kwanza mno kuzungumza kazi mpya ya Tikisa ya Q Chief mara tu ilipotoka. (Wimbo)

Na hatukuwa wanafiki bali kueleza kweli yenye kweli juu ya ubora wa wimbo huo katika upana wa Q Chief ambapo daima ni bora. (Ujuzi)

Na pitapita ya mahojiano katika sehemu nyingi za Media ni safi zaidi tukaona ni mwanzo mzuri wa Q Chief katika muendelezo imara. (Nyakati)

Leo ni katika fadhaiko imara la Q Chief hasa ni katika lalamiko la kubaniwa tena na mtu mmoja au wawili ambao hakuwaweka wazi. (Soni)

Nani akubanie? na kwanini akubanie? ni nani anaweza kuzuia vyote katika nchi hii? kama ni mtangazaji mmoja katika Radio mosi kwanini hutumii Radio pili? (Ajabu)

Unalalama nini? na ili iweje? kwanini huo muda wa malalamiko usitangaze kazi yako ya Tikisa katika ukubwa? (Kabisa)

Umri wako si wa kulalama kama mtoto mdogo na wa kambo, bali ukomavu wa majungu na fitina za muziki katika muendelezo imara. (Naam)

Kabisa nguvu kubwa iwe katika lalamiko? mbona unashangaza kaka yetu Q Chief ni sawa na yule ambaye anauza Ng’ombe na kununua bakora.(Chekesho)

Acha malalamiko juu ya kituo chochote cha Radio au Runinga bali vituo vingine katika kutangaza kazi zako. (Hakika)

Kushindwa ni wewe kujiwekea imani bila mahala fulani huwezi kusonga mbele, hakika huo ni upuuzi katika mafikirio. (Amka)

Muziki wako na kipaji chako ni kikubwa usitie huruma katika unyonge wa fedheha mbele ya jamii bali ukomavu katika mapambano ya muziki na endelezo. (Ndiyo)

Lakini daima “Macho hayana thamani kama akili ina upofu” (Tafakarii)

#MuzikiNiSisi

 

Malalamiko ya Q Chief ni katika mtandao wa picha katika ukurasa wa Bongo Five