Pink na Chemical Achana na mimi ni wimbo uliowashusha kisanii.

Pink na Chemical Achana na mimi ni wimbo uliowashusha kisanii.

Wakati wote waswahili husema “mwenye kelele hana neno” kwa hakika ni kwa uhakika.

Kabla ya kutoka kwa wimbo wa Achana na Mimi  tulijionae kelele za kwenye mtandao wa picha “Instagram” kati ya Chemical na Pink ambapo walikuwa ni watu wa majibizano ikiwa ni kutengeneza kusikika na kila mmoja.

Na baada ya muda mfupi wakatoa wimbo ambao unamilikiwa na Pink na wimbo huo umefanywa na mtayarishaji Mbezi.

Ni wazi waswahili hawakukosea kusema “Mshale usiyo na nyoya haundi mbali”. Katika uhalisia wimbo huu wa Achana na mimi hauwezi kwenda mbali kwa maana ni wimbo ambao hauna kiwango cha biashara kwa sasa.

Lakini ikumbukwe uchache wao marapa wa kike kwenye hiphop imekuwa ni wepesi mkubwa wa kupewa nafasi. Lakini je!kwa wimbo huu utapewa nafasi?

Maana nyakati hizi ni lazima wimbo uwe umetima katika mambo yafanyayo wimbo uwe wimbo katika ubora.

Kwa maana ya mdundo, midondoko, mistari lakini uchanganyaji. Ni wazi wimbo huu umekosa mambo yote hayo. Haitupi shida kusema wimbo huu umewashusha kisanaa wasanii hawa.

Na hapa hakuna wakumlaum Zaidi ya nafsi zao lakini mtayarishaji. Wimbo huu unaonyesha kwa namna ambavyo wasanii hawakuwa tayari lakini nguvu ya mahusiano kati ya mtayarishaji Mbezi  na Pink imechangia kufanya kitu hiki ambacho ni kibaya kwenye uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Ni vyema kukaa na kujipanga tena maana waswahili husema “Mpiga ngumu ukuta huumiza mkonowe”

 

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa