Perfomance ya Mwasiti na G Nako ni maana halisi ya wimbo bora.

Perfomance ya Mwasiti na G Nako ni maana halisi ya wimbo bora. 

Daima “Mwenye kulinda utambuzi atapata mema”, Lakini kuujua utambuzi wenye kutambua vya kutambua ni kazi ngumu. (Hakika)

Ni wazi dada yetu kipenzi Mwasiti utambuzi wake katika ujuzi wa kufanya muziki unafanya kuendelea kuwepo kila leo. (Naam)

Mwasiti ametambua yakuwa “Muziki ndiyo nguzo kuu” vivyo daima simamio lake ni katika muziki wenye uhalisi tangu kuchipuka kwake mpaka leo. (Muda)

Wimbo wake wa Perfomance akiwa na G Nako umeonyesha namna ya Mwasiti ni mtambuzi imara katika tungo zenye tafsida kuu lakini uimbaji wenye kukosha sikio katika usikivu. (Mpangilio)

Lakini tupendacho zaidi ni Mwasiti yule yule asiyechosha katika usikivu wa nyimbo tangia tangu na tangu ya Nalivua Pendo mpaka Perfomance. (Uhalisia)

Ilihali uwepo wa G Nako umeleta kolezo zuri lenye ujazo wa ladha kamili ya wimbo huu. Ikumbukwe G Nako ni mithili ya ala ya muziki inayopiga katika shairi lolote. (Ujuzi)

Ila Aloneym amefanya kazi bora na kubwa katika mdundo huu wenye ladha yetu katika bongo fleva imara. (Usikivu)

Yote ya yote Mwasiti anabaki kuwa msanii wetu bora katika uwanja huu wa muziki, hili halina mjadala kwetu sisi wajuzi wenye maana kuu ya kusimamia muziki. (Upekee)

Ni wazi Perfomance ni wimbo wenye ukamili kuanzia ngazi ya Tungo, Uimbaji, Mdundo lakini hata changanyo. (Muziki)

Na tunapenda mjue enyi mashabiki yakuwa “Huu ni mfano halisi wa wimbo bora katika nyakati hizi za kujali kutrendi zaidi mitandaoni kwa matukio” (Naam)

#MuzikiNiSisi #ZimaKikiWashaMuziki