Pah One hawakuwa na lakufanya zaidi ya kifuniko cha Jibebe ya Wasafi.

Pah One hawakuwa na lakufanya zaidi ya kifuniko cha Jibebe ya Wasafi.

Ni wazi Pah One hali yao kimuziki kwa sasa si njema na zaidi ni yenye ubaya wa fedheha katika anguko lao la muziki.

Na hakika wanatupa maana halisi ya semi ya mswahili yakuwa “Nyakati hupita”. Lakini daima “Chombo cha kuzama hakina usukani”.

Pah One hawakupaswa kufanya ‘Cover’ ya Jibebe kwa upana wao ambao walikuwa. Bali kazi zao katika nguvu ambayo wametumia kuitangaza Jibebe hakika ingekuwa vyema.

Ikumbukwe hakuna kiwango cha msanii katika upana wa kufanya Cover. Ila kusoma alama za nyakati ni jambo jema zaidi.

Wajuzi wameshindwa kufumba vinywa vyao juu ya Pah One katika kifuniko cha Jibebe ya Wasafi. Wajuzi wanaamini yakuwa ni endelezo la anguko lao maana hakuna ambaye atazingatia Cover yao bali wimbo kamili wa Jibebe.

Na wajuzi wanaamini Pah One wamepotoka mno katika kufanya hivyo, la! hasha wangesimama katika upana wao wa kufanya kazi zao.

Kwa nafasi ambayo walikuwa haipaswa na si sawa kutegemea tegemeo la Cover ya Jibebe, bali ngoma zao zenye ujazo kamili kama Pah One katika nyakati zao zenye ukamili.

Daima “Kawia ufike” Pah One wanapaswa waishi katika semi hii ya mswahili. Ni vyema wachukue muda katika utoaji wimbo wao na ukitoka uwe wenye ujazo kamili si kutaka Cover iwape nafasi katika uwanja wa muziki wa sasa.

Ni vyema tafakari iwepo katika halia ya muziki ya Pah One. Ni wazi walikuwa safi katika nyakati fulani na wakitulia hakika wanaweza kurudi tena kwa uzuri.

#TuzungumzeMuziki