P Funk Majani na kivuli cha hayati Mwalimu Nyerere.

p-funk_majani

P Funk Majani na kivuli cha hayati Mwalimu Nyerere.

Nyakati za kupata uhuru mwaka 1961 kutoka mikononi mwa muingereza kila mtanganyika alikuwa na maana yake juu ya neno “uhuru”. Hapa wapo wale ambao waliamini kuwa vita ya unyanyaswaji itakuwa imeisha kabisa.

Mwalimu Julius Nyerere yeye alikuwa tofauti na wengi katika tafsiri ya neno “Uhuru”. Kwa upande wake yeye aliamini “uhuru” ni “kazi”. Akiwa na maana baada ya kuwaondoa wakoloni hakuna kingine zaidi ya kazi katika kujenga nchi.

Kwa mwenendo wa uongozi bora Mwalimu Nyerere anabaki kuwa kiongozi bora katika bara la Afrika. Sifa kubwa ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ni katika ukweli na uwazi na kujali maslahi ya kila mmoja kwa nafasi yake.

Tukirudi katika muziki wetu wa kizazi kipya yani bongo fleva/hiphop sasa umekuwa chachu ya ajira kwa vijana walio wengi. Licha ya kuwepo kwa changamoto ambazo hazina msingi wala maana.

P Funck Majani ni moja kati ya watayarishaji wenye heshima kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi pia . Sifa ya ukweli na uwazi ni sifa ambayo P Funck Majani ameweza kuwa nayo.

Ni miaka ya 1990 na kuendelea ndio alianza kujishughulisha na muziki wa kizazi kipya. Lakini sifa ya ubabe wenye tija ni sifa yake kubwa, ila sifa ya kujali maslahi ya kila msanii ni sifa pekee ambayo anayo tangu mpaka sasa. Na ameshapigania haki za wasanii na bado anaendelea kupigania haki hata leo hii.

Haikuwa ni kificho kwa P Funk kukuelezea kuwa hujui kuimba na wakati huo ukiwa umeshika pesa yako ukihitaji kurekodi katika studio yake ya Bongo Records. Na hata kukueleza uende ukajifunze au uachane na muziki, lakini si kuchukua pesa yako tu imradi kama wafanyavyo watarishaji wengi wa sasa.

Bongo Record ni studio yake ambayo mpaka sasa ndiyo studio inayoongoza kutoa “hits songs” kuliko studio yoyote hapa Tanzania. Lakini pia katika upande wa album, licha ya kuwa ni studio lakini iliweza kuwa na Label kubwa hata kufikia hatua ya kuweza kufanya tour mbalimbali za ndani ya nchi. Hapa nazungumzia Bongo Records Tour ambayo ilikuwa miaka ya 2004.

Mauzo ya album yamefanya wasanii wengi kujipatia kipato cha kutosha na kuendeleza maisha yao pamoja na familia zao. Haikumpa shida P Majani kumchukua msanii husika na kumpeleka mpaka kwa msambazaji ili asaini mkataba yeye msanii na sio yeye Majani.

Jay Mo ni moja kati ya wa wasanii wengi waliowahi kunithibitishia hilo ambapo aliniambia “Amini usiamini Batro, Majani hakuwa na longo longo hata kidogo yani anakuchukua mpaka kwa mamu na unasaini mwenyewe mkataba aiseh” Itaendeleaaa

Tufuate Twitter Tizneez

Facebook Tizneez

Instagram Tizneez