One The Incredible amemaliza kazi yake, sasa ni zamu yenu mashabiki.

One The Incredible amemaliza kazi yake, sasa ni zamu yenu mashabiki.

Sisi ni miongoni mwa watu ambao tulikuwepo katika uzinduzi wa Ep yake usiku wa jana pale Element.

Na masikio yetu yalipata kusikia ilihali macho yakiona kwa uzuri namna ya One alivyoweza kutumbuiza nyimbo zake ambazo zipo kwenye Ep.

Na tumbuizo lake lilikuwa ni kwa bendi ya Trinity Idea, ambapo walifanya kwa ukubwa wa hali ya juu.

Na waswahili hunena yakuwa “Shahidi ndiye mwenye neno” Basi kwa uhalisi na uhalisia huu yapasa tunene hadharani neno letu.

Ni wazi Ep ni nzuri kupita kiasi na jambo jema ni kwamba yapatikana katika ngazi ya mtandao.

Hivyo popote ulipo unaweza kuipata na kufurahia Ep hii.

Na “mwenye sifa yake mpe” kwa hekima ya mswahili basi waache tuisema kweli yenye kweli juu ya One.

One The Incredible anabaki kuwa bora kati ya wasanii wachache wenye uwezo mkubwa wa kutumia bendi.

#TuzungumzeMuziki