One Incredible na Fid Q na ukweli halisi juu ya Ze City.

One Incredible na Fid Q na ukweli halisi juu ya Ze City.

Daima waswahili husema “Shahidi ndiye mwenye neno” na haitupi shida kuhuburi neno ambalo mara nyingi hulisikia kutoka kwa One The Incredible na Fid Q juu ya Ze City.

Ze City ni  moja kati ya marapa wa kike wakali ambao katika vilinge vyote vya hiphop amekuwa ni gumzo.

Uwezo wake ni mkubwa na amekuwa akisimama mbele ya kundi la wasanii wa kiume wa hiphop na mara nyingi huibuka kinara, na hii ni katika yale majukwaa ya hiphop ambayo daima watu wa hiphop hupendelea kwenda.

Hapa tunazungumzia jukwaa kama Open Mic na Movement Cypher (Kilinge).

Katika majukwaa haya Ze City huwa ni msichana pekee mwenye kuudhuria mara nyingi Zaidi na wakati wote hufanya vyema.

Kujiamini, midondoko, mitindo huru na uandishi, ni mambo manne ambayo One The Incredible na Fid Q wamekuwa wakisifu uwezo wa dada huyu wakati wote.

One The Incredible aliwahi kusema “Sijawahi kuona rapa wa kike kwenye huu muziki mwenye uwezo kama Ze City, hebu tumpe support huyu ana kitu kikubwa mno”

Lakini wakati huo Fid Q amekuwa akiongea mara kwa mara kwenye jukwaa lake la Open Mic kukiri uwezo wa Ze City. Lakini huonekana mwenye furaha na kushangilia vyema mara tu Ze City awapo jukwaani.

Ukweli huu juu ya uwezo wa Ze City ni wazi watu hawa wanao, lakini hakuna kingine ambacho kitaweza kumfanya Ze City kufahamika Zaidi nje ya vilinge hivi kama watu wa Media hawajaamuza kuzungumza kuhusu muziki wake.

Ze City anastahili nafasi kubwa kwa maana ana kitu kikubwa cha kuweza kuongeza kwenye muziki huu wa kizazi kipya.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa