Ommy Dimpoz Yafaa awe na tofauti ya utendaji wa kimuziki na Ali Kiba.

Ommy Dimpoz Yafaa awe na tofauti ya utendaji wa kimuziki na Ali Kiba.

Cheche ni wimbo wake wa kwanza kutoa akiwa chini ya Rockstar 4000 Record label, ambapo katika uhalisia si wimbo ambao uliweza fanya vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Na wimbo huo ulitoka mwezi wa 9 mwaka 2017. Lakini ikumbukwe Ommy Dimpoz ni msanii ambaye alikuwa/anamiliki Label yake ambayo ni PKP na Nedy Music ni msanii wake wa kwanza kusaini.

Shangazo la watu wengi ni yeye kusaini RockStar 4000, ilihali watu wanapaswa kujua si dhambi msanii kumiliki Label na yeye kusainiwa na Label nyingine. Duniani kote hilo swala lipo na huwa wazi.

Ila katika uhalisia Ommy Dimpoz ameshuka kimuziki si kupanda kama wengi wadhaniavyo. Na sababu kubwa ya yeye kushuka kimuziki ni yeye kutaka kufuata njia apitayo Ali Kiba katika utoaji nyimbo.

Lakini ingekuwa vyema mno kama yeye angekuwa na utofauti katika utendaji wake kimuziki na Ali Kiba licha ya kufanya kazi katika nyumba moja. Kwa hakika angefanikiwa mno.

Waswahili husema “Mwenye njaa hana miiko” Na ni wazi yafaa kusiwe na miiko katika ufanyaji kazi hasa kwenye muziki wetu wa kizazi kipya. Hususani miiko ya kutoa wimbo mmoja kwa miezi, 3, 6 au mwaka.

Maana muziki wetu ni muziki ambao kila leo wasanii wakubwa wamekuwa wakitoa kazi, hivyo kitendo cha yeye kuwa kimya ni wazi hakimsaidii maana mashabiki hawakosi cha kusikiliza.

Lakini yafaa ajue yakuwa “Mvumbika changa hula mbovu”. Kwa hakika ukimya wake kwenye muziki utamgharimu kwa maana mashabiki wa muziki wa kizazi kipya ni wepesi mno kuhamisha sikio.

Lakini ingekuwa ni jambo jema na zuri kwake kujitahidi walau kuweka vipande vya video walau akiwa studio kwa maana waswahili husema “Ushikwapo shikamana”

Lakini kuendelea kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa ni mwenye kwenda mbio na muenekano wake ni wazi haina faida kimuziki. Ni vyema ajue watu wanapenda mno kazi zake na sio muonekano wake kwa uhakika.

 

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa