Ommy Dimpoz karibu tena katika uwanja wa muziki

Ommy Dimpoz karibu tena katika uwanja wa muziki.

2018 ulikuwa ni mwaka mgumu zaidi kwa msanii Ommy Dimpoz. Ambapo upasuaji wa mara tatu ulikuwa juu ya mwili wake. (Maradhi)

Ukimya ulikuwa tawala katika muziki wake, na hakika ni jambo ambalo halikupendeza kwa wengi. (Mipango ya Mungu)

Leo hii tunaona namna afya yake imetengemaa vyema, huku wimbo wake wa “Ni wewe” ukiwa umeanzisha siku ya leo. (Naam)

Kutoa wimbo wenye kueleza magumu ambayo amepitia ni jambo zuri mno. Wimbo huu kila usikilizapo hisia za upole na huruma lazima ziwe juu ya wewe. (Kweli)

Ni wimbo mzuri mno na kamilisho la sauti ya Bella inazidi kukonga nyoyo kwa upana wake. (Hakika)

Na sasa Ommy Dimpoz amerejea rasmi katika uwanja wa muziki, kuanza na wimbo wa aina hii ni vyema.

Tizneez tunamtakia yote yenye kheri katika muziki huu. Muda ni wako fanya kwa uwezo wako Ommy Dimpoz. (Karibu)

#MuzikiNiSisi