Nuh Mziwanda shika njia yako na uende zako.

Nuh Mziwanda shika njia yako na uende zako.

Daima husisitiza yakuwa muziki una nguvu kuliko matendo yasiyo na upana wa muziki. Na mwisho wa matendo hayo hubaki fedheha kwa msanii mbele ya wajuzi na jamii.

Miaka mitatu nyuma Nuh hakuwa msanii mwenye kuheshimika na wajuzi bali fedheha tu . Na hii ni kutokana na hali ya kuendekeza ya hovyo kuliko muziki wake.

Ila nyakati hizi ni wazi amezitupa hovyo na kuweka simamio la hakika juu ya muziki wake. Na ukumbusho halisi wenye uhalisi ni wimbo wake wa ‘Jike Shupa’.

Na nyakati hizi ni ‘Kitu na box’ akiwa na Ben Paul ni uhalisi wa uhalisia wa upana wa muziki wake na kipawa chake katika ujazo wa wimbo wake.

Nuh ameonyesha mikao ya uimbaji katika wimbo wake huu, mbinu ya utoaji wa sauti yake yenye ukamili ambayo si katika muigo wa magharibi.

Lakini hatuwezi kusahau mbinu ya utaamkaji wa maneno katika nogesho la kuleta ukamili wa wimbo huu katika lugha yenye ladha tamu ya usikivu kwenye masikio.

Koleza la ala hakika limefanya sikio lisikie usikivu mzuri wa wimbo bora wenye ujazo kamili.

Naam! kwetu sisi wimbo umepitishwa katika upana wa ubora wa sasa na nyakati zijazo. Ni vyema kushika njia yako hii ya muziki na uende zako na muziki wako.

Muziki utaishi bali matendo hupita na watu wake, basi ni vyema Nuh Mziwanda ushike njia yako ya muziki na uende zako.

#TuzungumzeMuziki