Nini kinashindaka juu ya hili la Roma?

Nini kinashindikana katika hili la Roma?? maana simu zinapatikana kipi kinashindikana kujua Roma na Moni wapo wapi?? Mbona kama watu waki wakashifu viongozi huwa ni jambo dakika kujua huyo mtu yuko wapi?

Jambo hili ni jambo baya, lakini je wahusika wa mamlaka zote kuhusu jambo hili wanajua jinsi mitaa inavyolia kuhusu Roma??

Nawakumbusha tu “Wanyonge wakichoka wanageuka waasi,tena bila wasiwasi”

Je wanataka tufike huko?? Wanahubiri eti tuidumishe amani,sasa amani ina faida gani wakati vijana wanapotea katika mazingira ya kazi zao?? lakini ni aina gani ya maumivu wanayopata familia yao?

Inasikitisha sana jambo hili,ila niliwahi kuandika makala ambayo inasema “Wasanii wanaangamia kwa kukosa maarifa” makala hii iliandikwa 2016. Na katika uhalisia ni kwamba wasanii wana nguvu kubwa mno katika mitaa yote, lakini cha ajabu hawajui nguvu yao.

Kama wataamua kuungana kwa nguvu zote jambo hili si kubwa, wakiamua kwa namna ipi? hili ni swali la wengi, Kuweka posti katika mitandao ya kijamii lakini hata kuanda maandamano/Makutano ya kutaka mwenzao ajulikane alipo.Wasanii mnapaswa mjue “Uoga hauna msaada zaidi ya kukuvuruga akili”

Nguvu ya wasanii iko wapi??kweli mpaka leo wapo wasanii ambao wapo kimya katika kuposti kuhusu Roma na Moni,tunajua kama uoga wa kimaslahi yao juu ya urafiki na watu kadhaa.Lakini inapaswa kujua “Uoga hauna msaada zaidi ya kukuvuruga akili”

Ni jambo la kushangaza zaidi,Basata ambao mnasema ni walezi wa wasanii swala la Roma likoje kwenu??Au kazi yenu ni kufungia nyimbo??

Nikki Mbishi aliwahi kusema katika wimbo wake wa Natokea Tanzania “Nchi ambayo haitambui mchango wa wasanii” haya yanatokea sasa, Kama nchi ingekuwa inatambua basi swala la Roma lingeshugulikiwa kwa wepesi sana, ila Karibu tanzania nchi ambayo Mnyama akipotea anaundiwa tume ila binadamu watu wanakaa kimya tena ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii.

Roma aliwahi kusema “Wanatugawa kimafungu ili watumeze”

Kukaa kimya kwa wasanii sio njia ya kumsaidia Roma,ila pazeni sauti zenu kukemea upuuzi huu pazeni sauti zenu maana zina nguvu.Hamuoni wanawatumia kwenye majukwaa yao ule muda ukifika?? maana ni wazi mna nguvu Pazeni sauti wasanii wote bila kujali.

Wasanii si huwa mnapiga picha na viongozi huku mmeshika glasi za juice sasa mbona hawawapi ushirikiano katika hili?

#NchiHiiHakiHakunaMabomuYaMachoziNaMajiYaKuwashaIpoSikuYaFyata

Hivi kuhusu Roma inabidi tuombe atafutwe au ni lazima vyombo husika vimtafute?

Wasanii ambao mnajitambua hongereni sana na tuendelee kupambana juu ya Roma pia sanaa kwa jumla,waacheni tu makay wajikombe kombe.

“Watanzania hatuna amani tunadanganywa”

 waFreeRoma #VivaRoma 

Umoja ni Nguvu Oii