Nini kinaendelea kwenye maisha ya Sanaa ya Shaa?

Nini kinaendelea kwenye maisha ya Sanaa ya Shaa?

Shaa ni moja kati ya wadada ambao waliweza kuongeza kasi ya ushindani na chachu nzuri ya muziki huu wa kizazi kipya.

Shaa ambaye wimbo kama Sugua gaga ulimfanya aweze kutambulika Zaidi kwenye ramani ya muziki.

Ukimya wake umekuwa ni mkubwa sasa, ambapo kila mmoja amekuwa akihoji hasa nini kinaendelea katika maisha yake ya Sanaa?

Kwa maana hata katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ni wazi amekuwa akiendelea kuweka maisha yake nje ya Sanaa tofauti na mwanzo. Jambo la kuwa kimya bila kusema jambo lolote kuhusu Sanaa yake ni wazi anazidi kupotea kisanaa.

Sanaa ya sasa ni Sanaa ambayo imechangamka mno ambayo inahitaji kazi kila baada ya muda mfupi. Hivyo uongozi wake yapasa itazame jambo hili kwa maana bila umakini ni wazi kipaji hiki kitapita kama upepo wa bahari ya hindi kwenye fukwe zake.

Uwanja wa muziki wa kizazi kipya ni wazi bado unamuhitaji Shaa, hivyo ni vyema kusema jambo lolote lenye matumaini kwa mashabiki wake maana kusema jambo litaondoa maswali mengi ambayo yapo kichwani mwa mashabiki wengi.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa