Nikki wa Pili ni somo kwa wasanii wachanga na wakubwa pia.

Nikki wa Pili ni somo kwa wasanii wachanga na wakubwa pia.

Leo Nikki wa pili kila mahala amekuwa akichomoza vyema, na wapo ambao wamekuwa wakiamini yakuwa ni katika upendeleo.

Ni wazi si upendeleo bali ni katika nidhamu ya kazi na kusimamia misingi ya sanaa ya muziki, si kuyumbishwa na upepo ambao haufai katika mambo ya hovyo.

Lakini wepesi wake katika ushiriki wa mengi yenye kuelemisha jamii kwa hali ya upana, kimsingi ni msingi wa sanaa ya muziki ulivyo katika uhalisia wake

Na leo anatoa soma kubwa na rahisi kabisa katika kueleweka.

“Somo kwa wasanii Wachanga, usichukulie poa unayo yafanya mtandaoni hujui nani anayaona, kabla huja tafuta kiki kwa mambo yasiyo mazuri waza mara mbili.

Sikuwahi kujua kuwa Mkurugenzi wa bank ya DCB ni mmoja kati ya watu wanao nifuatilia mtandaoni”

Mswahili anena “Shika shika lingali kichwani” Je!unadhani ni watu wangapi katika makampuni wanafuatilia msanii na sanaa kwa ujumla?

Msanii usiiwaze leo na kesho waza kwa upana katika kesho kutwa ya nje ya sanaa ama ndani ya sanaa.

#TuzungumzeMuziki