Nikki wa Pili ishi katika uisho wa maneno ya Joh Makini.

Nikki wa Pili ishi katika uisho wa maneno ya Joh Makini.

Tupo katika kizazi ambacho walio wengi ni wapingaji ambao hata hawajui wanapinga nini katika kile ambacho wanapinga. Ni Soni kubwa maana ‘Hawajui na hawajui kama hawajui’ (Fedheha)

Lakini kwa hekima ya uisho wa mswahili hatuna shangazo wala gadhabu ya upingaji wao wa hoja nyingi zenye kweli na uhalisi. Maana semi kuu ya mswahili yanena yakuwa “Mpumbavu asipoelewa jambo hugadhibika, bali mwerevu hukuna kichwa”.

Hakika tupo na wapumbavu wengi katika kizazi cha mtandao. (Uhalisi). Werevu wenye tafakari ya hoja ni katika kundi dogo mno. (Soni)

Imekuwa shangazo kwetu katika lugha kali juu ya Nikki wa pili kunena hadharani yakuwa “Ndoto yangu ni kuja kuwa Rais”. Na ajabu ni kundi kubwa kutokea na kumpinga vyema.

Hivi wanapinga nini? Na ni wapi inakatazawa mtu kunena ndoto yake? Je!upana wa lugha kali juu ya ndoto yake nini upi?. (Chukizo).

Walitaka anena uongo wa ndoto yake?. Hakika hawakuwa na upana wa tafakari wenye kupinga ndoto ya mtu. Hakika wapingaji ni wale wenye kulala na kuishi ndoto zao na sio wenye mikakati katika upana kufikia ndoto zao.

Lakini sisi ni wale wenye kuunga mkono ndoto ya Nikki wa pili, na tunakuunga vyema  maana kuishi katika ndoto yako ni jambo jema.

Na hata Joh Makini katika wimbo wa ‘I see me’ ananena yakuwa “Ndoto sio kuzikalia skani mkilialia/ Ndoto ni kuamka mbio kuzikimbilia’.

Semi hii ina maana kubwa katika ndoto, hakuna ambacho anapaswa Nikki wa pili kufanya zaidi ya kuishi katika uisho wa maneno haya ya Joh Makini. Na hapa ni kuzikimbilia ndoto zake katika njia kuu ambayo itaweza kumfikisha vyema katika uisho kamili wa ndoto yake ya kuwa Rais.

Baraka za Tizneez uko nazo kaka yetu Nikki wa pili, na ukatimize ndoto yako katika upana wa maisha yako.  Wakatishaji tamaa katika ndoto yako ujue hawana ndoto ya lolote wala chochote zaidi mtandao.

Na hao ni mfano wa uhalisi wa uhalisia wa wafu maana daima “Mfu ndiye asiye na ndoto bali aliyehai” (Uhalisi)

#TuzungumzeMuziki