‘Ni vyema tujifunze kuielewa sanaa ya muziki si kukosoa usichojua’ Dogo Janja

‘Ni vyema tujifunze kuielewa sanaa ya muziki si kukosoa usichojua’ Dogo Janja

Sanaa ya muziki ina upana mkubwa tofauti na wengi wanavyoifikiria kwa urahisi.

Na moja ya sifa ya msanii katika sanaa ya muziki ni kuweza kuvaa uhusika wa hisia zake ambazo anataka kuwasilisha kwa hadhira. (Uhusika)

Na moja ya makosa makubwa ya walio wengi sasa kushindwa kuelewa ujumbe ambao msanii ametaka kuwasilisha. (Kosa)

Na matokeo yake wanakazania kwa mapana kuangalia makosa, na kugeuka wakosoaji wasio na ujuzi. (Tokeo)

Na nyakati zote “Kukosoa jambo usilolijua ni makosa” (Uhakika)

Shangazo ni kukosoa wimbo wa Dogo Janja wa ‘Banana’ hivi mtu unakosoa upande upi?. Tukumbuke nyakati hizi ni za audio mbaya video nzuri. (Uhalisi)

Lakini Dogo Janja amefanya yote kwa ujazo kamili wa ukamilisho wa wimbo. Kwa maana ya audio nzuri na video nzuri katika kiwango cha juu.

Ambacho tumependa zaidi ni aina ya uimbaji wake ambapo inaonyesha namna ya anavyokuwa kisanaa kila iitwapo leo.

Ni wazi Banana si wimbo wa kukosolewa hata kwa udogo bali kusifiwa kwa mapana yake, katika kweli yenye kweli Dogo Janja ameweza kwenda sawa katika kusaka mashabiki wapya kwa aina ya muziki wake katika upya huu.

Ikumbukwe nyakati zote biashara inahitaji ongezeko la wanunuzi (Mashabiki) hivyo kusimamia upande mmoja wa biashara huleta matata nyakati fulani.

Na hatuachi kuwakumbusha kumbukumbu yakuwa “Sanaa ya muziki ni ufundi ambao anatumia msanii ili kuwasilisha fikra/mawazo yaliyoko ndani yake, vilevile Sanaa ya muziki ni uzuri unaojibua katika umbo lililosanifiwa.

Ilihali kusanifu ni kuumba au kufanya jambo au kitu kwa kutumia ustadi ili kiweze kuvutia kwa hadhira, Je! wimbo wa ‘Banana’ hauvutii kwenye usikivu wa sikio?

Hakika kwenda na nyakati lakini kuzijua dakika vyema kutafanya Dogo Janja kuendelea vyema kukua na kujitangaza vyema kisanaa.

Pongezi ziwe kwako Dogo Janja hakika wengi sasa wanapenda ‘Banana’. Na mswahili hunena yakuwa “Tofauti yenye tofauti huleta tofauti” Ilihali “Kuelewa pia ni kipaji”

#TuzungumzeMuziki