Ni vyema kuwe na chaguzi la nyimbo za kupiga mbele ya watoto

Ni vyema kuwe na chaguzi la nyimbo za kupiga mbele ya watoto.

Wajuzi wanatujuza yakuwa “Muziki unaweza kubadilisha watu maana unabadilisha Dunia” Na hii uhalisi kulingana na nguvu ya muziki.

Na hata katika nyakati za harakati katika ukombozi wa mengi muziki ulitumika zaidi katika kuhamasisha.

Mwanzo wa muziki huu katika miaka 1990- ilikuwa ni tungo zenye uimara mkuu. Vivyo mafundisho yalikuwepo haswa.

Achilia mbali mafundisho, pia ikumbukwe dhima kuu ya muziki ni burudani kuu. Sasa ya muziki yenye burudisho kuu na mafundisho ya hovyo katika tungo.

Hii haina shida katika sanaa kwa ujumla, shida ni pale ambapo tungo za hovyo zinapokuwa ni kuu mbele ya watoto. 

Tunaona wasanii wengi sasa hupita katika shule za msingi na sekondari lakini hata kwenye matamasha ya watoto pia hushiriki.

Lakini katika ushiriki wao hucheza nyimbo ambazo si sawa na umri wa watoto katika ukuaji wao.

Ikumbukwe watoto ni wenye upana wa kushika vitu kwa urahisi mno, vivyo tungo zenye lugha kali kana kwamba watu wapo disko si njema mbele ya watoto.

Na uhalisia ni kwamba ni kheri waandaji wa shoo za watoto na maeneo ya shule kutazama zaidi maudhui yenye kulenga watoto zaidi.

Si maudhui yenye ujazo wa tungo za watu wazima na iwe ni ushiriki watoto. Ni vyema kulitazama hili kwa mapema zaidi.

Na kama msanii unaona kuna fursa yenye uhitaji katika soko la watoto basi tengeneza nyimbo zenye maudhui katika watoto. 

Ila kuimba nyimbo zenye ujazo wa tungo zenye hamasisho la ngono na pombe ni kuharibu zaidi watoto na kesho kuwa ni mbaya zaidi.

Ni kheri tutumie nyimbo sahihi katika nyakati sahihi, tusitumie nyimbo ilimradi, tutafakari katika kesho ya mtoto itakuaje? 

#MuzikiNiSisi